Pata taarifa kuu
ALGERIA-USHIRIKIANO

Algeria yaimarisha diplomasia yake kuokoa muda uliopetea katika enzi ya Bouteflika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Algeria Ramtane Lamamra, kiongozi mwenye uzoefu na mwenye bidii katika masuala ya kidiplomasia nchini Algeria, Alhamisi wiki hii alitangaza kuzifutia deni nchi 14 za Afrika, kitita kilicho karibu na dola bilioni moja.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra, Machi 20,2020.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra, Machi 20,2020. AFP - ODD ANDERSEN
Matangazo ya kibiashara

Ishara hii ya uhusiano wa kidiplomasia inaelezwa na Algiers kama ishara ya "msikamano wa dunia". Algeria haizitaji nchi hizo. Mpango huu umeongezwa kwa nchi zingine zilizopewa deni na Algeria kupata ushawishi wake wa zamani.

Diplomasia ya Algeria inatarajia kupata tena ushawishi "kuimarisha jukumu lake kama nguvu ya kati". Kulingana na ofisi ya rais wa Algeria, Algeria lazima iwe "na uwezo wa kuchukua hatua juu ya maswala makubwa ya kikanda na kimataifa". Katika siku za hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amekuwa akifanya ziara nyingi katika nchi mbalimbali za Afrika.

Nchini Niger, alijadili na rais Bazoum kuhusu"kazi ya pamoja ya kulinda amani na usalama barani Afrika". Kulikuwa pia na mazungumzo juu ya kufufua tena makubaliano ya usalama yaliyotiwa saini mnamo mwaka 2018 kati ya Niger, Libya, Chad na Sudan. Ramtane Lamamra pia alikuwa nchini Mauritania kumualika rais Ghazouani huko Algiers.

Wiki iliyopita, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi jirani za Libya wote walikutana huko Algiers kujadili juu ya hali ya utulivu kwa nchi hiyo. Mchakato huu wa nchi jirani uliositishwa tangu Januari 2020 ulizinduliwa tena na Algiers kutetea njia ya kuiondoa Libya kwa mgogoro huo mbali na kuingiliwa kwa yoyote ya kigeni.

Lamamra pia amehusika kama mpatanishi katika mzozo wa Bwawa la Renaissance la Ethiopia na alizuru Tunisia mara tatu tangu Julai 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.