Pata taarifa kuu
ALGERIA-USHIRIKIANO

Algeria yatangaza kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia na Morocco

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne, Agosti 24, 2021, kwamba Morocco inajiandaa "kuchukua hatua za uhasama" dhidi ya nchi yake. Algiers imetangaza kuvunjika kwa uhusiano wake wa kidiplomasia na Rabat

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Algiers, Agosti 24, 2021.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Algiers, Agosti 24, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

"Algeria imeamua kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Ufalme wa Morocco tangu leo", amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Ramtane Lamamra, wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria ametetea chaguo la serikali yake na kusema kuwa "historia inaonyesha kuwa ufalme wa Morocco haujawahi kusitisha kufanya vitendo vya uhasama dhidi ya Algeria".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.