Pata taarifa kuu
ALGERIA

Algeria yamrejesha nyumbani balozi wake Morocco

Wizara ya mambo ya nje ya Algeria imemrejesha nyumbani balozi wake nchini Morocco kupinga kauli ya mwakilishi wa Morocco katika Umoja wa Mataifa akitetea haki ya kujitawala kwa jimbo la Kabylia, kujibu uungwaji mmkono wa Algiers kwa wanaharakati wanaotaka wa jimbo la Sahara Magharibi wanaotaka kujitawala.

Wanajeshi wa jeshi la Algeria wakipiga doria kwenye milima ya Djurdjura huko Kabylia, Oktoba 2014.
Wanajeshi wa jeshi la Algeria wakipiga doria kwenye milima ya Djurdjura huko Kabylia, Oktoba 2014. AFP PHOTO / FAROUK BATICHE
Matangazo ya kibiashara

Sahara ya zamani chini ya utawala wa Uhispania katika enzi za ukoloni imekuwa, tangu katikati ya miaka ya 1970,  eneo la mzozo kati ya wanaharakati wanaotaka kujitawala wa Polisario Front na Morocco, ambayo inadhibiti na kutawala Sahara Magharibi na inaiona kuwa ni sehemu muhimu ya ardhi yake.

Kufungwa kwa mipaka ya ardhini kati ya Algeria na Morocco tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Algeria katika miaka ya 1990 kumezidisha mvutano kati ya majirani hao wawili, na kusababisha mizozo ya kidiplomasia.

Siku ya Jumapili wizara ya mambo ya nje ya Algeria ilibaini kwamba inaweza kuchukua hatua zaidi za kulipiza kisasi dhidi ya Morocco.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.