Pata taarifa kuu
ALGERIA

Abdelaziz Bouteflika azikwa kwenye makamburi ya mashujaa ya El Alia

Rais wa zamani wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amezikwa Jumapili hii Septemba 19 kwenye makaburi ya El Alia huko Algiers, yaliyotengwa kwa mashujaa wa Vita vya Uhuru, lakini hakupata heshima zote sawa na watangulizi wake.

Vikosi vya usalama vya Algeria vikisindikiza jeneza la rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika kwenda kwenye makaburi ya El-Alia katika mji mkuu wa Algiers Septemba 19, 2021.
Vikosi vya usalama vya Algeria vikisindikiza jeneza la rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika kwenda kwenye makaburi ya El-Alia katika mji mkuu wa Algiers Septemba 19, 2021. Ryad KRAMDI AFP
Matangazo ya kibiashara

Msafara wa magari ya yamewasili kwenye makaburi ya El Alia, baada ya kusafiri kilomita thelathini kutoka Zeralda, mji ulio magharibi mwa Algiers, ambapo alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 84. Mwili wake ulibebwa kwenye behewa lililovutwa na gari la kivita lililofunikwa maua.

Pamoja na wanafamilia, Rais Abdelmadjid Tebboune, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu chini ya utawala wa Bouteflika, mawaziri wa mambo ya nje na wanadiplomasia walikuwepo kwenye kaburi hilo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

Abdelaziz Bouteflika alizikwa kwenye Uwanja wa Mashahidi ambapo watangulizi wake walizikwa, ikiwa ni pamoja na mashujaa wa Vita vya Uhuru (1954-1962).

Wakuu wote wa zamani wa Algeria walipewa heshima zote rasmi za mazishi na siku nane za maombolezo ya kitaifa, kama rais wa kwanza wa Algeria huru Ahmed Ben Bella (1963-1965) na rais wa tatu wa nchi hiyo Chadli Bendjedid (1979-1992), wote wawili walifariki dunia mnamo mwaka 2012.

Bila kusahau mazishi makubwa ya rais wa zamani Houari Boumedienne (1965-1978), ambaye kabla ya mazishi yake mizinga mia moja ilipigwa mwaka 1978 na mamia ya maelfu ya watu walikusanyika kwa kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.