Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA

Zambia kufanya uchaguzi Alhamisi, hofu bado yatanda

Mmoja wa wagombea urais kupitia chama cha upinzani MMD nchini Zambia, Nevers Mumba, amekanusha madai kuwa amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais wakati wananchi wa Zambia wanapojiandaa kupiga kura siku ya Alhamisi.

Raia wanajiandaa kupiga kura Zambia kumchagua rais wao mpya na wabunge.
Raia wanajiandaa kupiga kura Zambia kumchagua rais wao mpya na wabunge. FP PHOTO / GIANLUIGI GUERCIA
Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa, Nevers Mumba, alikuwa amejiondoa na kuamua kumuunga mkono mgombea wa chama tawala cha Patriotic Front, kinachoongozwa na rais Edgar Lungu anayetafuta muhula mwingine.

Wagombea kumi na sita watapambana katika uchaguzi wa urais, lakini wawili ndio wanapewa nafasi kubwa katika uchaguzi huo: rais anayemaliza muda wake Edgar Lungu, wa chama cha Patriotic Front, na Hakainde Hichilema, wa chama cha United Party for National Development (UPND), ambaye anawania mara ya sita.

Edgar Lungu na Hakainde Hichilema watachuana Alhamisi kwa mara ya tatu.

Zambia iko katika hali ya sintofahamu siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu Alhamisi, Agosti 12, 2021. Angalau watu watatu waliuawa katika makabiliano kati ya wafuasi mwishoni mwa jumahili. Vurugu hizo zilisababisha kupelekwa kwa jeshi katika maeneo mbalimbali nchini humo Agosti 1.

Hivi karibuni Maaskofu nchini Zambia walitoa wito kwa raia wote kupiga kura kwa amani na kuepuka vurugu ili kufikia malengo ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.