Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Mvutano nchini Zambia kuhusu eneo la kuzikwa kwa Kenneth Kaunda,

Ndugu wa mwanzilishi wa nchi ya Zambia Kenneth Kaunda, wamekwenda Mahakamani kupinga kuzikwa kwake kwenye makaburi yaliyotengewa marais jijini Lusaka.

Mazishi ya kitaifa yaliyofanyika Julai 2 2021?  katika uwanja wa mashujaa jijini Lusaka
Mazishi ya kitaifa yaliyofanyika Julai 2 2021? katika uwanja wa mashujaa jijini Lusaka AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kaunda aliyefariki dunia Juni 17, akiwa na umri wa miaka 97, anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano, baada ya ibada ya kitaifa kufanyika wiki iliyopita katika uwanja wa mashujaa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa barra Afrika.

Watoto na wajukuu wa Kaunda wanataka Mahakama kuagiza, mpendwa wao kutozikwa katika êneo hilo maalum.

Wanataka Kaunda azikwe pembezoni mwa kaburi la mke wake Betty Mutinkhe Kaunda aliyefariki dunia mwaka 2012 kwa kuheshimu matamanio yake.

Serikali ya Zambia haijatoa tamko juu ya suala hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.