Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA

Uchaguzi-Zambia: Rais Lungu atuma jeshi katika maeneo mbalimbali

Zikiwa zimesalia wiki zisizozidi mbili kabla ya uchaguzi wa urais na wabunge Agosti 12, rais wa Zambia Edgar Lungu ametangaza kwamba ameagiza jeshi kwenda kusaidia polisi katika maeneo mbalimbali ili kupunguza vurugu za kabla ya uchaguzi. Mashirika ya kiraia yanalaani uamuzi huo yakisema kuwa ni jaribio la "kibabe" linalolenga kunyamanzisha upinzani.

El presidente de Zambia, Edgar Lungu, en Lusaka, el 6 de julio de 2017
El presidente de Zambia, Edgar Lungu, en Lusaka, el 6 de julio de 2017 Salim Dawood AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

"Nimeagiza Jeshi la Zambia, Jeshi la Anga la Zambia na idara za usalama nchini Zambia kusaidia polisi kushughulikia hali ya usalama". Rais wa Zambia Edgar Lungu, amebaini kwamba kutumwa kwa wanajeshi kusaidi polisi kunalenga "kudhibiti vurugu za kisiasa" zilizoonekana katika siku mbili zilizopita. Katika mji mkuu Lusaka na pia katika majimbo mengine, wafuasi wa chama tawala na wapinzani walikabiliana na, wakati mwingine, walitumia mapanga na mashoka.

Je! Ilikuwa ni lazima kupeleka jeshi kote nchini?

Kwa vyovyote vile, kulingana na wasomi kadhaa na maafisa wa mashirika ya kiraia nchini Zambia, wakinukuliwa na shirika la habari la AFP, wamebaini kuwa hali hiyo haiendani uamuzi huo wa rais Lungu na wameshtumu "hatua ya kukatisha tamaa inayowatishia wapiga kura".

Edgar Lungu, aliyechaguliwa katika uchaguzi uliozua utata mwaka 2016, sasa anawania muhula wa pili. Mpinzani wake mkuu, Hakainde Hichilema, amekamatwa mara kadhaa tangu atangaze kugombea urais.

Mnamo mwezi Juni, shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International tayari lilionyesha ukandamizaji "wa kikatili" uliofanywa na rais Edgar Lungu dhidi ya wapinzani wote, na kuitaja Zambia kama nchi "ambapo haki za binadamu ziko katika mgogoro".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.