Pata taarifa kuu
ZAMBIA - MAZISHI

Viongozi mbalimbali watua Lusuka kuhudhuria ibada ya wafu ya Kaunda

Viongozi wa tabaka  mbalimbali wamewasili nchini Zambia kuhuduria hafla ya kitaifa ya ibada ya wafu  ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Kenneth Kaunda.

Aliyekuwa rais wa Zambia,Kenneth Kaunda
Aliyekuwa rais wa Zambia,Kenneth Kaunda © Patrick Durand/Sygma via Getty images
Matangazo ya kibiashara

Mpiganiaji huyo wa uhuru wa Zambia alifariki akiwa na umri wa miaka 97 kutokana na pneumonia.

Jeshi la Zambia limekuwa likiusafirisha mwili wa Kaunda, katika mikowa yote 10 ya taifa hilo ili raia watoe heshima zao za mwisho kwa shujaa huyo wa Africa.

Rais wa Zambia, Edgar Lungu, ametangaza leo na siku ya jumatano siku itayozikwa Kaunda kuwa sikuku ya kitaifa.

Hafla ya mazishi ya Kaunda itahudhuriwa na familia yake na viongozi wachache waliakwa siku ya jumatano juma lijalo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.