Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA

Sintofahamu yatanda Zambia kabla ya uchaguzi mkuu

Zambia iko katika hali ya sintofahamu siku nne kabla ya uchaguzi mkuu Alhamisi, Agosti 12, 2021. Angalau watu watatu wameuawa katika makabiliano kati ya wafuasi. Vurugu hizo zilisababisha kupelekwa kwa jeshi katika maeneo mbalimbali nchini humo Agosti 1.

Jeshi la Zambia linashika doria katika mitaa ya mji mkuu Lusaka, wakati wa kunaripotiwa ghasia nyingi kabla ya uchaguzi mkuu Alhamisi Agosti 12.
Jeshi la Zambia linashika doria katika mitaa ya mji mkuu Lusaka, wakati wa kunaripotiwa ghasia nyingi kabla ya uchaguzi mkuu Alhamisi Agosti 12. © SALIM DAWOOD/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wagombea kumi na sita watapambana katika uchaguzi wa urais, lakini wawili ndio wanapewa nafasi kubwa katika uchaguzi huo: Rais anayemaliza muda wake Edgar Lungu, wa chama cha Patriotic Front, na Hakainde Hichilema, wa chama cha United Party for National Development (UPND), ambaye anawania mara ya sita.

Edgar Lungu na Hakainde Hichilema watachuana Alhamisi kwa mara ya tatu. Uchunguzi uliochapishwa kuhusiana na uchaguzi huo unatoa takwimu tofauti. Katika uchunguzi wa kwanza, Lungu anapewa ushindi kwa 44% ya kura. Takwimu zilionekana kuwa nzuri sana kwa baadhi ya wachambuzi, na ambazo zilikataliwa na uchunguzi wa pili. Uchunguzi wa pili unampa Hichilema ushindi kwa 24%.

Vurugu na hofu

Lakini wengi wa waliohojiwa wanakataa kuonyesha ni nani watakayempigia kura, ishara ya kuongezeka kwa hofu ambayo inaashiria uchaguzi huu. Kwa wiki moja, jeshi limekuwa likifanya doria katika mitaa ya Lusaka kudumisha utulivu, baada ya vifo vya wafuasi watatu wa vyama vya kisiasa, wakiwemo wawili kutoka chama tawala. Lakini upinzani, kama waangalizi wengi, wana hofu kuwa askari watatishia wapiga kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.