Pata taarifa kuu
BURUNDI-USHIRKIANO

Burundi na DRC kusaini mikataba mbalimbali ya kibiashara

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye anazuru nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na baada ya kuwasili jana Jumatatu hivi leo anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Félix Tshisekedi jijini Kinshasa.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye AFP - TCHANDROU NITANGA
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya rais Ndayishimiye jijini Kinshasa, ni jitihada za rais Tshisekedi, kuimarisha ujirani mwema, baada ya wiki kadhaa zilizopita, kukutana na rais wa Uganda Yoweri Museveni na Paul Kagame wa Rwanda.

Taarifa zinasema, viongozi hao wawili katika kikao chao watajadiliana kuhusu ujenzi wa reli kati ya Gitega upande wa Burundi na Kindu nchini DRC na kusaidia usafirishaji wa bidhaa na watu.

Aidha, wanatarajiwa kuanzisha tena tume ya pamoja kuangazia masuala mengine tata kati ya nchi hizo mbili, baada ya kutokutana kwa kipindi kirefu.

Suala la usalama wa Mashariki mwa DRC linatarajiwa pia kutawala mazungumzo hayo, kufuatia kuwepo kwa makundi yenye silaha kutoka Burundi yaliyokimbilia mkoa wa Kivu Kusini, lakini pia kuendelea kuwepo kwa wakimbizi wa Burundi nchini DRC wapatao 45,000, linatarajiwa kujadiliwa.

Tangu kuingia madarakani kwa rais Thisekedi, wanajeshi wa Burundi wameripotiwa kuvuka mpaka na kuingia mashariki mwa DRC mara kadhaa kwa mujibu wa ripoti ya watalaam wa Umoja wa Mataifa iliyochapishwa mwezi Januari mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.