Pata taarifa kuu
BURUNDI-AFYA

Burundi-DRC: Pesa za kupima COVID-19 kwenye mpaka wa Gatumba zazua mvutano

Mpaka wa Gatumba kati ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umefunguliwa tena tanu Jumanne wiki hii baada ya kufungwa mwaka uliopita kwa sababu ya maambukizi ya Covid 19, lakini kumeibuka mvutano kuhusu gharama inayotozwa kupima maambukizi hayo.

Polisi katika eno la Gatumba, magharibi mwa Burundi, kwenye mpaka na DRC Septemba 15, 2018.
Polisi katika eno la Gatumba, magharibi mwa Burundi, kwenye mpaka na DRC Septemba 15, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada tu ya wasafiri wa kwanza kuvuka mpaka na kuingia nchini Burundi na kuombwa walipe kiwango cha dola 30 ambazo ni gharama ya kipimo cha virusi vya  Corona, wengi baadhi yao wamesema pesa hiyo inayoombwa ni nyingi mno.

Waziri wa Burundi wa Afya Thaddée Ndikumana anasema hana uwezo wa kupunguza gharama hiyo ya kipimo cha virusi vya  corona na amekumbusha kwamba raia wa Burundi wanavuka mpaka huo watatakiwa kulipa Franga za Burundi 15, 000 na dola 30 kwa raia kutoka DRC.

Upande wa DRC, ofisi ya idara ya uhamiaji katika eneo la Kavimvira imeisha chukua uamzi wa kuwaomba raia warundi wanaorejea nyumbani kulipa kila moja dola 10 badala ya 5.   

Raia hao warundi walionekana wakihangaika kati ya kituo cha mpakani cha Kavimvira upande wa DRC na kituo cha Gatumba upande wa Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.