Pata taarifa kuu
BURUNDI-DRC

Mpaka wa Gatumba wafunguliwa tena baada ya kufungwa kudhibiti maambukizi ya Corona

Mpaka wa Gatumba kati ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umefunguliwa tena baada ya kufungwa mwaka uliopita kwa sababu ya maambukizi ya Covid 19, lakini kumeibuka na mvutano kuhusu gharama inayotozwa kupima maambukizi hayo.

Polisi katika eno la Gatumba, magharibi mwa Burundi, kwenye mpaka na DRC Septemba 15, 2018.
Polisi katika eno la Gatumba, magharibi mwa Burundi, kwenye mpaka na DRC Septemba 15, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Magari yanaonekana yakiingia na kutoka kutoka pande zote za mpaka wa Gatumba, baada ya kuwasili wanatakiwa kulipitia gharama ya kupata kipimo cha haraka cha maambukizi ya corona na hapo ndio mvutano unazuka.

 Kufungua ya leo, itatusaidia vipi wakati hatuvuki. Hatuna ile Dola 30 wanayotaka, sijui tutafanya nini. Kwa namna hali ilivyo Burundi haifungua chochote kwa sababu mimi sioni kama nitaweza kuvuka, mmoja wa wafanyibiashara kutoka DRC amesema.

Waziri wa Burundi wa Afya Thaddée Ndikumana anasema hana uwezo wa kupunguza gharama hio ya kipimo cha virusi vya  corona na ni  Faranga za Burundi  15, 000 kwa raia wa Burundi, na Dola 30 kwa raia wa DRC.

Tunaomba Burundi ishushe bei, DRC wanaomba Dola tano sawa na Rwanda, inakuwaje sasa, huu ni ujirani wa ainga gani ? Hatutembeleani.

Upande wa Kongo, idara ya uhamiaji ya Kavimvira imesema raia wa Burundi wanaorejea nyumbani sasa watalipa Dola 10  kutoka Dola 5.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.