Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Burkina Faso: Watu zaidi ya 100 wauawa katika shambulio Solhan

Watu wenye silaha wamewauwa karibu raia 100 katika shambulio la usiku katika kijiji kimoja kaskazini mwa Burkina Faso, serikali imesema leo Jumamosi.

Jeshi la Burkina Faso linaendelea kkabiliana na makundi yenye silaha.
Jeshi la Burkina Faso linaendelea kkabiliana na makundi yenye silaha. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji walitekeleza shambulio katika kijiji cha Solhan katika mkoa wa Yagha mpakani na Niger, na kuua watu kadhaa na kuchoma nyumba na soko, serikali ya Burkina Faso imeongeza.

Serikali imewaelezea washambuliaji kama magaidi, lakini hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo hatari.

Uvamizi wa wanajihadi wanaohusishwa na Al Qaeda na kundi la Islamic State (IS) katika ukanda wa Sahel umeongezeka tangu mwanzoni mwa mwaka huu, hasa nchini Burkina Faso, Mali na Niger, huku vifo zaidi vikiripotiwa upande wa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.