Pata taarifa kuu
BURKINA FASO

Kumi waangamia katika shambulio kaskazini mwa Burkina Faso

Mashambulio mabaya yalitekelezwa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne dhidi ya vijiji kadhaa katika mji wa Seytenga, kaskazini mwa Burkina Faso, na kuua "watu kumi" kulingana na serikali, "kumi na tano" kulingana na afisa mteule wa eneo hilo.

Vikosi vya usalama vya Burkina Faso vyapiga doria. (Picha ya kumbukumbu.)
Vikosi vya usalama vya Burkina Faso vyapiga doria. (Picha ya kumbukumbu.) AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Jumanne jioni, Aprili 27, Waziri wa Mawasiliano wa Burkina Faso na msemaji wa serikali, Ousséni Tamboura, alibaini katika taarifa kwa waandishi wa habari kamba kulitokea "uvamizi wa watu wenye silaha katika maeneo kadhaa ya Sahel - Sofokel, Yatakou, Tao na Seytenga - katika mkoa wa Séno".

“Magaidi wamefanya vitendo vya vitisho, uporaji na mauaji kwa raia. Watu kumi wameuaa katika shambulio hilo, ”alisema waziri huyo.

Afisa mteule katika eneo hilo ametaja watu 15 waliouawa katika shambulio hilo. "Watu wenye silaha wametekeleza shambulio katika vijiji  kadhaa katika mji wa Seytenga, na kuua watu karibu kumi na tano," afisa huyo ambaye hakutaja atajwe jina amelimbia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.