Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Burkina Faso: Kumi na tano waangamia katika mashambulizi mawili Adjarara

Karibu raia kumi na tano na mwanajeshi mmoja waliuawa Jumanne na Jumatano katika mashambulio mawili kwenye kijiji kimoja cha wilaya ya Tin-Akoff na atu wenye silaha kaskazini mashariki mwa Burkina Faso, kulingana na vyanzo vya usalama.

Jeshi la Burkina Faso linaendelea kukabiliana na mashambulizi ya makundi yenye silaha.
Jeshi la Burkina Faso linaendelea kukabiliana na mashambulizi ya makundi yenye silaha. © REUTERS/LUCGNAGO
Matangazo ya kibiashara

Shambulio la kwanza lililenga usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano kijiji cha Adjarara, katika manispaa ya Tin-Akoff, Kaskazini mwa nchi, na kusababisha "watu kumi na tano kufariki dunia". Shambulio jingine la bomu limelenga msafara wa jeshi mashariki mwa nchi na kusababisha kifo cha askari mmoja.

"Wilya ya Tin-Akoff imelengwa tena na watu wenye wasiojulikana ambao walishambulia kijiji cha Adjarara jana (Jumanne, usiku). Ripoti ya awali inabaini kwamba karibu watu kumi na tano waliuawa kati ya watu ambao walikuwa wakisherehekea ubatizo," chanzo cha usalama kimeliambia shirika la habari la AFP.

Mei 12, jeshi la Burkina Faso lilitangaza kwamba liliharibu ngome ya magaidi katika eneo la Tin-Akoff.

Burkina Faso imekuwa ikikabiliwa tangu 2015 na mashambulio ya mara kwa mara na mabaya ambayo yanatekelezwa na makundi ya kijihadi, ikiwa ni pamoja na kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (lenye mafungamano na Al-Qaeda) na kundi la Islamic State huko Grand Sahara na kusababisha watu milioni moja kuyatoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.