Pata taarifa kuu
LIBYA-URUSI-UN-USALAMA

Ripoti: Urusi yaongeza msaada wake kwa mamluki nchini Libya

Urusi imeongeza msaada wake wa vifaa vya jeshi kwa kundi la mamluki nchini Libya kwa kutuma meli kadhaa za kijeshi zinazosheheni vifaa vya kijeshi, katika miezi ya hivi karibuni, kusaidia mamluki kutoka kampuni binafsi ya Urusi, inayosaidia majeshi ya Jenerali Khalifa Haftar, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Majeshi ya Khalifa Haftar huko Bengazhi. (Picha ya kumbukumbu).
Majeshi ya Khalifa Haftar huko Bengazhi. (Picha ya kumbukumbu). Abdullah DOMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo, iliyoandikwa na wataalam huru na kuwasilishwa kwa Tume ya inayofuatilia vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Libya- lakini bado haijawekwa wazi - pia imebaini kwamba Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu, Jordan, Urusi na Qatar zimekiuka sheria za vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Libya, juu ya uuzaji wa silaha.

Nchi za Jordan, Urusi, Qatar, Uturuki na Umoja aw Falme za Kiarabu hazijatoa maelezo yoyote kuhusiana na madai hayo. Mwezi Januari rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa kama kuna raia wa Urusi wako nchini Libya, watu hao hawajawakilisha nchi hiyo wala hawalipwi na serikali ya Urusi.

Libya imegawanyika mara mbili tangu mwaka 2014. Serikali inayotambuliwa kimataifa inatawala Tripoli na kaskazini magharibi mwa nchi, wakati vikosi vya Marshal Haftar vinadhibiti mashariki mwa nchi hiyo. Vikosi vya mbabe huyu wa kivita vilitekeleza mashambulizi dhidi ya mji mkuu Tripoli mwaka jana, lakini vilitimuliwa na kurejea kwenye ngome zao, mashariki mwa nchi hiyo.

Kulingana na ripoti hiyo, takriban ndege 338 za kijeshi za mizigo ziliondoka nchini Syria kwenda Libya kati ya mwezi Novemba na Julai kusaidia wapiganaji kutoka kampuni binafsi ya kijeshi ya Wagner Group.

"Usaidizi wa moja kwa moja wa vifaa vya kijeshi kutoka Urusi kwa kundi la ChVK Wagner, na labda makundi mengine ya mamluki kutoka Urusi, (...) umeongezeka sana kati ya mwezi Januari 2020 na Juni 2020", ripoti hiyo imebaini.

Katika ripoti ya siri ya mwezi Mei, waangalizi wa Umoja aw mataifa walisema kuwa kundi la Wagner Group lina karibu wapiganaji 1,200 waliotumwa nchini Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.