Pata taarifa kuu
MAURITANIA-SIASA

Mauritania: Rais mpya ateua mawaziri wa serikali yake

Rais mteule wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani, ambaye alishinda uchaguzi wa Juni 22 mwaka huu, ameteua mawaziri wa serikali yake ya kwanza.

Rais mteule wa Mauritania, Mohamed Ould Ghazouani, wakati wa kuapishwa kwake, Agosti 1, 2019 Nouakchott.
Rais mteule wa Mauritania, Mohamed Ould Ghazouani, wakati wa kuapishwa kwake, Agosti 1, 2019 Nouakchott. © Seyllou / afp
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya kwanza ya Rais Mohamed Ould Ghazouani ni sawa na ile iliyokuepa katika utawala wa Mohamed Ould Abdel Aziz. Hakuna mwanasiasa wa upinzani ambaye ameshirikishwa katika serikali hiyo mpya.

Pamoja na kuwa Rais Ghazouani amewateua maafisa waandamizi kadhaa wanaojulikana, kama kamishna mkuu wa zamani wa Shirika la Maendeleo la Mto Senegal, ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya ndani, au Haimoud Ould Ramdane, wakili anayeshughulikia masuala ya kutetea haki za binadamu ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Sheria.

Wengine ni pamoja na Jenerali Hanena Ould Sidi, kamanda wa jeshi la pamoja la ukanda wa Sahel, G5 Sahel, ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi, na Taleb Ould Sid'Ahmed, mwandishi wa zamani wa televisheni ya serikali na afisa mwandamizi katika Benki ya Dunia nchini Cote d'Ivoire, ameteuliwa kuwa Waziri wa Vijana na Michezo.

Kwa upande wa mawaziri waliokutwa katika serikali ya Ould Abdel Aziz, Rais Ghazouani amemuachia Ismail Ould Cheikh Ahmed kwenye nafasi yake ya Mambo ya Kigeni na Nani Ould Chrougha kwenye Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa majini. Naye Mohamed Abdel Vetah amesalia kwenye nafasi yake ya Mafuta.

Serikali hii imeteuliwa siku kumi baada ya Rais Ghazouani kuapishwa. Miongoni mwa changamoto zinazomkabili ni pamoja na marekebisho ya mfumo wa elimu na usambazaji bora wa rasilimali za kitaifa kwa wananchi wote wa Mauritania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.