Pata taarifa kuu
MAURITANIA-UCHAGUZI-SIASA

Upinzani wafutilia mbali matokeo ya uchaguzi Mauritania

Upinzani nchini Mauritania umekataa kutambua matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita ambapo mgombea wa chama tawala, alitangazwa mshindi.

Wagombea wanne wa upinzani katika mkutano na waandishi wa habari. Kutoka kushoto kwenda kulia, Sidi Mohamed Ould Boubacar, Kane Hamidou Baba, Mohamed Ould Maouloud na Biram Dah Abeid.
Wagombea wanne wa upinzani katika mkutano na waandishi wa habari. Kutoka kushoto kwenda kulia, Sidi Mohamed Ould Boubacar, Kane Hamidou Baba, Mohamed Ould Maouloud na Biram Dah Abeid. équipe de campagne de Sidi Mohamed Ould Boubacar
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa siku ya Jumapili unatajwa kama ulikuwa uchaguzi wa kihistoria katika taifa hilo lililoko kwenye eneo la jangwa la Sahara, uchaguzi wa kwanza utakaoshuhudia ubadilishanaji wa madaraka kwa amani.

Hata hivyo mgombea wa upinzani Birahm Dah Abeid anasema uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu ambapo pia amekosoa hatua ya kukamatwa kwa wafuasi wa upinzani.

Mgombea wa chama tawala nchini Mauritania, Mohamed Ould Ghazouani alitangazwa mshindi wa kiti cha urais kwa asilimia 52 ya kura katika uchaguzi wa mwishoni mwa juma.

Kwa upande wao chama tawala kupitia mshauri wa masuala ya kisiasa wa rais mteule, Mohamed Salem Ould Merzoug anasema upinzani unayo njia moja tu nayo ni kwenda mahakamani kupinga ushindi wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.