Pata taarifa kuu
MAURITANIA-SIASA-USALAMA

Rais Abdel Aziz akabidhi madaraka baada ya miaka 11 ya uongozi ya nchi

Baada ya miaka kumi na moja madarakani, Mohamed Ould Abdel Aziz ananatarajia kukabidhi madaraka leo Alhamisi hii, Agosti 1 kwa Mohamed Ghazouani.

Rais Mohamed Ould Abdel Aziz Julai 2, 2018 Nouakchott.
Rais Mohamed Ould Abdel Aziz Julai 2, 2018 Nouakchott. Ludovic MARIN / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mohamed Ghazouani atakuwa na kibarua kigumu hususan kurejesha usalama na kuleta usawa kati ya wananchi.

Mohamed Ould Abdel Aziz amekuwa akiwapokea, katika dakika hizi za lala salama, viongozi kutoka nchi mbalimbali walioalikwa kwenye sherehe hiyo ya kuapishwa kwa rais mpya, ambaye ni mrithi wake.

Mapema Jumatano asubuhi, alijielekeza kwenye makao makuu ya mamlaka ya ukaguzi wa fedha kutangaza mali yake. Lakini mali ya rais Abdel Aziz iliyotangazwa baada ya kuondoka madarakani haikuelezwa kwenye vyombo vya habari.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron hatahudhuria kwenye sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya lakini amewakilishwa na mbunge Jean-Jacques Bridey.

Rais Mohamed Ould Abdel Aziz aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia, Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallahi, kabla ya kuandaa na kushinda uchaguzi wa urais wa 2009 kwa muhula wa miaka mitano, na kurejea tena katikauchaguzi wa urais wa mwaka 2014.

Katiba ya Mauritania inaruhusu tu mihula mawili kwa kuwa rais wa nchi hiyo. Lakini Abdel Aziz hajasema kuwa hatorejea madarakani. Mwanzoni mwa mwezi Juni alisema kuwa ataendelea kushiriki siasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.