Pata taarifa kuu
COMORO-SIASA

Mgawanyiko wajitokeza katika serikali kuhusu kura ya maoni Comoro

Makamu wa rais na magavana wawili nchini Comoro wamemuomba rais wa nchi hiyo Azali Assoumani "kuachana" na mpango wake wa kuitisha kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba iliyoyopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Julai.

Rais wa Comoros Azali Assoumani, wakati wa sherehe yake ya kutawazwa, Mei 26, 2016.
Rais wa Comoros Azali Assoumani, wakati wa sherehe yake ya kutawazwa, Mei 26, 2016. IBRAHIM YOUSSOUF / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mageuzi hayo ya katiba yanamruhusu rais Assoumani, ikiwa kura ya Ndiyo itashinda, kuwania muhula wa pili mfululizo.

"Rais angelipaswa kushauriana na viongozi waliochaguliwa juu ya kufanyika kwa kura ya maoni (...) Tungemshauri atathmini hali inayoweza kuibuka baada ya hatua hiyo (....) na kuachana na mpango wake huo kuhusu mageuzi ya katiba ambayo yanaweza kuitumbukiza nchi hii katika mgogoro wa mkubwa wa kisiasa, "wamebaini watatu hao waliotia saini kwenye barua walioandikia Umoja wa Afrika (AU).

Ujumbe wa AU Unazuru Comoro

Rais Azali alipanga kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba Julai 29 ili kurekebisha mfumo unaotoa nafasi kwa kila baada ya miaka mitano uongozi wa kisiwa hicho kuwaniwa na mgombea kutoka kwenye moja ya visiwa vyake vidogo vitatu (Anjouan, Grande-Comore, Moheli).

Kwa mujibu wa Makamo wa rais na magavana hao wawili waliotia saini kwenye waraka huo, mageuzi hayo "yanataka kuitenga Anjouan na Moheli kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais wa Comorokatika mwaka wa 2021 na 2026 kinyume na ahadi zilizotolewa" na " hivyo kusababisha mgawanyiko".

Rais Azali, ambaye alichaguliwa mnamo mwaka 2016, ni kutoka kisiwa cha Grande-Comore.

Barua hiyo imesasainiwa na Makamu wa Rais kutoka Grande-Comore, Ahmed Saïd Djaffar, Gavana wa Grande-Comore, Hassani Hamadi, na Gavana wa Anjouan, Abdou Salami Abdou.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.