Pata taarifa kuu
COMORO-UCHAGUZI-SIASA

Comoro: jina la rais mtarajiwa mikono mwa wapiga kura 6,000

Nchini Comoro, wapiga kura 6,300 wanatarajiwa kupiga kura leo Jumatano katika muendelezo wa uchaguzi wa urais ulioitishwa baada ya vurugu wakati wa duru ya pili ya uchaguzi. Kura ya uamuzi wa kuamua kati ya kiongozi wa zamani wa mapinduzi Azali Assoumani na mgombea wa utawala unaomaliza muda wake " Mamadou ".

Mwanamke huyo wa Comoro akiwa mbele ya orodha ya majina ya wagombea katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais Februari 22, 2015 Moroni.
Mwanamke huyo wa Comoro akiwa mbele ya orodha ya majina ya wagombea katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais Februari 22, 2015 Moroni. AFP/Aboubacar M'CHANGAMA
Matangazo ya kibiashara

Kanali Assoumani, ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi hiyo kuanzia mwaka 1999 hadi 2006, alikua akiongoza katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais wa Aprili 10, kwa 40.98% ya kura, kwa mujibu wa matokeo ya awali. Lakini anamshinda mshindani wake Mohamed Ali Soilihi "Mamadou" kura 2,000 tu sawa na 39.87% ya kura.

Duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Comoro ilikubwa na machafuko, hasa katika kisiwa cha Anjouan ambapo masanduku ya kura yaliharibiwa na watu kudhalilishwa katika vituo vya kupigia kura.

Jumla ya wapiga kura 6,305 katika vituo vya kupigia kura 13 hawakuweza kupiga kura, kwa mujibu wa Mahakama ya Katiba ambayo iliamuru kuandaa upya uchaguzi wa urais katika maeneo hayo ya Anjouan.

Uchaguzi huu mdogo wa leo Jumatano unaohusu 2% ya wapiga kura, unaweza kubadilisha matokeo ya mwanzo katika duru ya pili ya uchaguzi.

Jumatatu wiki hii, mbele ya vyombo vya habari, Azali Assoumani, alionyesha matumaini yake ya kushinda uchaguzi huo.

"Kama mifumo ya kupiga kura itakua salama, hakuna sababu ya mimi kutokua rais mwaka 2016, Inshallah," kanali Assoumani amesema.

Kanali Assoumani, aliyeingia madarakani katika mapinduzi ya mwaka 1999 kabla ya kuchaguliwa mwaka 2002, anapewa msaada muhimu na Rais wa zamani Ahmed Abdallah Sambi, kutoka Anjouan, ambapo ni maarufu sana.

Hatua za usalama zimechukuliwa ili kuzuia mdororo wa usalama ambao unaweza kutokea Jumatano hii, katika nchi ambayo imeshuhudia mapinduzi na majaribio ya mapinduzi zaidi ya ishirini tangu kupata uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1975. Polisi wa kutuliza ghasia wametumwa katika kisiwa cha Anjouan, ambapo Mkuu wa majeshi Youssouf Idjihadi ameelekea kuhakikisha usalama umeimarishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.