Pata taarifa kuu
COMORO-UCHAGUZI-SIASA

Comoro: zoezi la uhesabuji kura laanza

Nchini Comoro, zoezi la upigaji kura limemalizika katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais. Na kama katika mji mkuu, zoezi la upigaji kura lilifanyika bila vurugu, katika visiwa vingine viwili vya Anjouan na Moheli kulishuhudiwa vurugu.

Zoezi la kupiga kura katika mji wa Moroni, Comoro, wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais tarehe 10 Aprili, 2016.
Zoezi la kupiga kura katika mji wa Moroni, Comoro, wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais tarehe 10 Aprili, 2016. © IBRAHIM YOUSSOUF / AFP
Matangazo ya kibiashara

Karibu nchini kote, vituo vya kupigia kura vimefungwa. Baadhi vilisalia wazi baadaye kidogo ikilinganishwa na wakati uliokua umetolewa ili kuokoa muda uliokua umepotea Jumapili hii asubuhi. Hatimaye, zoezi la uhesabuji limeanza, huku wawakilishi wa wagombea wakishuhudia

Baada ya kujitokeza bnaadhi ya kasoro katika duru ya kwanza, Tume ya Uchaguzi imechukua hatua ya kuhakikisha uwazi zaidi. Kila mgombea amekua na mwakilishi katika vituo vyote vya kupigia kura tangu asubuhi na sasa wawakilishi hao wanaendelea kufuatilia zoezi la uhesabuji na kisha watapewa nakala ya ripoti zote ili kufanya hesabu zao wenyewe za matokeo.

Vurugu katika Anjouan na Mohéli

Katika kisiwa cha Ngazija, zoezi limefanyika kwa amani. Wakuu wengi wa vituo vya kupigia kura wameshuhudia kiwango cha nchini cha ushiriki. Lakini katika visiwa vingine viwili vya Comoro, kumekuwa na mvutano hadi baadhi ya ofisi kufungwa katika kisiwa cha Anjouan.

Mgombea Mouigni Said Baraka Soilih amehakikisha kwamba katika vijiji kadhaa vya kisiwa, masanduku ya kura hayakua tupu mapema mchana. Mgombea huyo amesema kuwa wafuasi wa chama tawala kisaha walijaribu kuvuruga zoezi hilo la kupiga kura ili kujaribu kufuta uchaguzi katika vituo vya kupigia kura ambavyo havikua upande wao.

Katika kisiwa cha Mohéli, wafuasi kadhaa wamekamatwa. Lakini wahusika wamehakikisha kwamba walilengwa tu kwa sababu wamekua wakiunga mkono mgombea wa mpinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.