Pata taarifa kuu
ANGOLA-UCHAGUZI

UNITA yawasilisha mashtaka mahakamani kupinga uchaguzi

Moja ya chama kikuu cha upinzani nchini Angola UNITA kimekimbilia mahakamani kupinga uchaguzi mkuu wa juma lililopita, kikisema uchaguzi huo haukuwa wa haki katika kura iliyoshuhudiwa chama cha rais wa zamani Jose Eduardo Dos Santos kikisalia madarakani.

raia wakipiga kura, Luanda, Angola, Agosti 23, 2017.
raia wakipiga kura, Luanda, Angola, Agosti 23, 2017. Lusa
Matangazo ya kibiashara

Chama tawala MPLA kilishinda uchaguzi huo kwa zaidi ya asilimia 61 na pia kuchukua viti 150 katika bunge lenye viti 220.

Katika uchaguzi huo mgombea wa chama hicho, Joao Laurenco alitangazwa mshindi .

Hata hivyo UNITA inasema itaenda mahakamani kupinga ushindi wake iliyosema ulichakachuliwa na kuwanyima upinzani nafasi kwenye vyombo vya habari.

Raul Manuel Danda ni makamu wa rais wa chama cha UNITA, anazungumza akiwa mjini Luanda, Angola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.