Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-COMPAORE-HAKI

Kesi ya rais wa zamani Blaise Compaoré kuanza kusikilizwa

Kesi muhimu nchini Burkina Faso inayomhusisha rais wa zamani wa nchi hiyo Blaise Compaoré inaanza kusikilizwa Alhamisi hii Aprili 27 mbele ya Mahakama Kuu ya mjini Ouagadougou.

Wakaazi wa mji wa Ouagadougou, Oktoba 31, 2014 wakiandamana kwa furaha baada ya kuanguka kwa utawala wa Blaise Compaoré.
Wakaazi wa mji wa Ouagadougou, Oktoba 31, 2014 wakiandamana kwa furaha baada ya kuanguka kwa utawala wa Blaise Compaoré. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Karibu mawaziri wote wa serikali iliyokua ikiongozwa na Waziri Mkuu Luc Adolphe Tiao wataripoti mahakamani kwa kuhusika katika ukandamizaji watu walioshiriki maandamano yaliyoanza mwezi Oktoba 2014ambayo yalisababisha kuanguka kwa utawala wa kiongozi huyo.

Rais wa zamani Blaise Compaoré, ambaye anaishi uhamishoni nchini Cote d'Ivoire na ambaye alipewa uraia wa nchi hiyo, atahukumiwa licha ya kutokuwepo Burkina Faso pamoja na Waziri wa zamani wa ulinzi.

Serikali iliokuwa ikiongozwa na waziri mkuu Luc Adolphe Tiao Inatuhumiwa kuhusika katika ukandamizaji wa waandamanaji mwaka 2014, walioshiniliza kuondolewa madarakani kwa rais Blaise Compaoré.

Kesi hii inaweza huenda ikadumu kwa takriban juma moja kwa mujibu wa duru za mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.