Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-COTE D'IVOIRE

Vibali vya kukamatwa dhidi ya Compaoré na Guillaume Soro vyafutwa

Mahakama Kuu ya Ouagadougou imefuta kibali cha kimaiafa cha kukamatwa kiliyotolewa na vyombo vya sheria vya kijeshi dhidi ya aliyekuwa Rais wa Burkina Faso Blaise Compaoré na Spika wa Bunge la Cote d'Ivoire Guillaume Soro, Mwanasheria Mkuu wa Mahakama hiyo amesema.

Wakazi wa Ouagadougou wakiweka vizuizi katika mitaa ya mji mkuu baada ya kutangazwa kwa mapinduzi ya serikali, Septemba 17, 2015.
Wakazi wa Ouagadougou wakiweka vizuizi katika mitaa ya mji mkuu baada ya kutangazwa kwa mapinduzi ya serikali, Septemba 17, 2015. © AFP PHOTO / AHMED OUOBA
Matangazo ya kibiashara

"Vibali vyote vya kimataifa vimefutwa leo na Mahakama Kuu kutokana na kasoro za utaratibu. Uamuzi huo unahusu vibali vyote vilivyokua vinalenga kumkamata Blaise Compaoré, Guillaume Soro na wengine," Mwanasheria Mkuu wa Mahakama, Armand Ouedraogo, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Uamuzi huo wa kufuta vibali hivyo umechukuliwa kutokana na kasoro za utaratibu kwa sababu ilikua inabidi kuomba maoni ya Kamishna wa serikali (Mwendesha mashtaka), maoni ya Mahakama ya kijeshi kabla ya kutoa vibali hivyo. Utaratibu huu haukutekelezwa, Mahakama imeamua kufuta vibali vyote vya kimataifa," Ouedraogo amesema.

Kamishina wa serikali amekiomba Baraza la udhibiti kisha Mahakama Kuu kwa kuweza kufuta vibali hivi, chanzo cha karibu na faili hii kimebaini.

"Ibara ya 130 ya Kanuni ya Jinai inamuagiza jaji maoni ya Mwendesha mashtaka kabla ya kutoa kibali chochote cha kimataifa cha kukamatwa," chanzo hicho kimesema.

Tarehe 4 Disemb 2015 vyombo vya sheria vya kijeshi nchini Burkina Faso vilitoa kibali cha kimataifa cha kukamtwa dhidi ya Blaise Compaoré, aliyekimbilia Cote d'Ivoire tangu utawala wake ulipoangushwa Oktoba 31, 2014.

Compaoré ameshitakiwa kwa kuhusika kwake katika mauaji ya Rais Thomas Sankara aliyeuawa Oktoba 15, 1987 wakati wa mapinduzi yaliyomueka madarakani.

Pia ameshitakiwa kwa "mauaji", ya raia wa Burkina Faso kama sehemu ya uchunguzi ulioanzishwa mwezi Machi 2015 na utawala wa mpito wa Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.