Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SHERIA

Gilbert Diendéré ashitakiwa kuhusika katika mauaji ya Thomas Sankara

Nchini Burkina Faso, jenerali Gilbert Diendéré, mkuu wa zamani wa kikosi cha usalama wa rais na mtu mwaminifu wa Rais wa zamani Blaise Compaoré, ameshtakiwa kwa akosa la "kushiriki" katika mauaji ya kapteni Thomas Sankara wakati wa mapinduzi ya Oktoba 15, 1987.

Jenerali Diendéré Gilbert mkuu wa zamani wa kikosi cha usalam wa rais na mshirika wa karibu wa Blaise Compaoré.
Jenerali Diendéré Gilbert mkuu wa zamani wa kikosi cha usalam wa rais na mshirika wa karibu wa Blaise Compaoré. AFP PHOTO / AHMED OUOBA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, jenerali Gilbert Diendéré ameshtakiwa kwa kosa la mauaji ya Rais Thomas Sankara. Jenerali Gilbert Diendéré anatazamiwa kueleza alichokifanya katika maandalizi na utekelezaji wa mapinduzi ya Oktoba 15, 1987, mapinduzi yaliogharimu maisha ya kapteni Thomas Sankara na washirika wake wa karibu kumi na mbili. Akithibitisha mashitaka ya mteja wake, wakili Mathieu Somé amebaini kwamba yuko tayari kuandaa utetezi wa jenerali Gilbert Diendéré.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwezi Oktoba mwaka jana, Mkuu wa Mahakama ya kijeshi alisema kuwa rais wa zamani Blaise Compaoré na mshirika wake wa karibu, jenerali Gilbert Diendéré, watafuatiliwa katika kesi ya mauaji ya kapteni Sankara mambo.

Wanasheria na familia ya Thomas Sankara bado wanasubiri matokeo ya vipimo vya DNA viliofanywa ndani ya kaburi linalokisiwa kuwa la Thoma Sankara. Uchunguzi ulionyesha kuwa mwili wa Thomas Sankara ulitobolewa na risasi alizopigwa wakati wa mapinduzi dhidi ya serikali yake. Kwa mujibu wa mwanasheria wa familia yake, rais alipigwa risasi wakati wa mapinduzi ya Oktoba 15, 1987.

Watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na askari kadhaa wa kikosi cha zamani cha usalama wa rais wameshitakiwa kwa kuhusika katika kesi hiyo. Kuhusu jenerali Gilbert Diendéré mashtaka yote hayajatangazwa rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.