Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UCHAGUZI-SIASA

Waziri mkuu wa zamani Roch Marc Kaboré anaongoza kwa kura Burkina Faso

Roch Marc Kaboré anaongoza kwa kura katika uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili mwishoni mwa juma lililopita nchini Burkina. Matokeo ya muda yameonyesha Jumatatu wiki hii kuwa Marc Kaboré anaongoza kwa 45% ya kura kutoka wilaya 368.

Roch Marc Kaboré anaongoza katika uchaguzi wa rais Burkina Faso.
Roch Marc Kaboré anaongoza katika uchaguzi wa rais Burkina Faso. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Matokeo haya ya muda, yaliyotangazwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, yanampa waziri mkuu wa zamani 55.3% ya kura dhidi ya 28.7% ya mpinzani wake mkuu, Zéphirin Diabré.

Kama matokeo haya yatathibitishwa, Roch Marc Kaboré atakuwa amechaguliwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais.

Wagombea kumi na wanne wanawania katika kinyan'ganiro hiki cha uchaguzi wa rais, lakini waangalizi wanaamini kwamba wawili tu kati yao wana uwezo wa kushinda, ikiwa ni pamoja na Roch Marc Kaboré, kutoka chama cha MPP, ambaye alikuwa waziri mkuu wa Rais Blaise Compaoré aliyen'gatuliwa mwaka uliyopita, na mfanyabiashara Zéphirin Diabré, kwa tiketi ya chama cha UPC.

Katika taarifa yake, Katibu mkuu wa muungano wa kimataifa wa nchi zinazozungumza Kifaransa, Michaëlle Jean, amekaribisha kufanyika kwa uchaguzi wa rais na wabunge ili kumaliza mgogoro nchini Burkina Faso.

"Raia wa Burkina Faso mara nyingine tena wameonyesha dhamira yao ya kina na demokrasia kwa kupiga kura kwa amani, Jumapili hii, Novemba 29, kwa kuwachagua wabunge wao na rais wao mpya kufuatia uchaguzi wa kihistoria", Michaëlle Jean amesema.

"Natoa wito kwa wagombea wote na vyama vya siasa lakini pia raia wa Burkina Faso, kuheshimu na kutekeleza matokeo ya uchaguzi yanayotangaza mara kwa mara na vyombo husika", Michaëlle Jean ameongeza.

Awali uchaguzi huu ulipangwa kufanyika Oktoba 11, lakini uliahirishwa kutokana na mapinduzi ya kijeshi Septemba 17, mapinduzi ambayo yaliongozwa na mtu wa karibu wa Blaise Compaoré, jenerali Gilbert Diendéré na kushindwa utokana na msimamo wa raia na majeshi tiifu kwa Rais Michel Kafando.

Matarajio ni mengi katika nchi hii maskini ya Afrika Magharibi yenye wakazi walio chini ya milioni 20, ambayo inataka kuona katika uchaguzi huu mwanzo wa kipindi chenye misingi ya kidemokrasia.

Watu milioni 5.5 waliojiandikisha kupiga kura wameitwa kushiriki katika uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa wabunge, kabla ya kubadili ukurasa wa utawala wa mpito uliowekwa baada ya maandamano makubwa yaliomng'oa madarakani Blaise Compaoré mwezi Oktoba mwaka 2014, wakati ambapo alikua akijaribukuifanyia marekebisho Katiba ili aweze kuwania muhula mwengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.