Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA-SIASA

Burkina Faso: changamoto za uchaguzi wa Novemba 29

Askari wasiopungua elfu 25 wa vikosi vya usalama wamesambazwa nchini Burkina Faso ili kuhakikisha uchaguzi wa rais wa Jumapili Novemba 29 unakuwa salama.

Kipindi cha mpito, chini ya uongozi wa Michel Kafando (ifikapo Novemba 1), kitakua kimefikia tamati kwa uchaguzi wa Novemba 29, 2015.
Kipindi cha mpito, chini ya uongozi wa Michel Kafando (ifikapo Novemba 1), kitakua kimefikia tamati kwa uchaguzi wa Novemba 29, 2015. © AFP PHOTO / AHMED OUOBA
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hizi zimetolewa Alhamisi wiki hii na Waziri wa usalama wa Burkina Faso, Alain Zagré Burkina, akihojiwa na shirika la habari la Ufaransa la AFP na kubainisha kuwa lengo ni kuzuia athari yoyote ya mashambulizi katika nchi hiyo ya Ukanda wa Sahel yenye wakazi milioni 20, na mpaka mrefu na nchi ya Mali ambapo mashambulizi yalitokea dhidi Hoteli Radisson Blu mjini Bamako tarehe 20 Novemba.

Vituo viwili vya polisi katika eneo la kaskazini vimeshambuliwa mwezi Agosti na Oktoba ambapo kumekuwa na mauaji kila wakati pamoja na utekaji nyara katika eneo la kaskazini, mashambulizi yanayowahusisha wanajihadi kulingana na vyanzo vya kidiplomasia.

Waziri Zagré amebainisha kuwa askari na wanajeshi wastaafu wanapiga doria usiku na mchana kwenye maeneo ya mipakani kuepuka tishio la ugaidi kutoka nje ya nchi hiyo, huku askari wa Ufaransa wa operesheni barkhane wakichangia kwa usalama wa Burkina Faso, ameongeza waziri huyo.

Wagombea kumi na wanne wako mbioni kwa ajili ya uchaguzi wa rais siku ya Jumapili, ambapo kipindi cha "mpito" kitafikia tamati yake tangu baada ya kuangushwa kwa aliyekuwa rais kwa takriban miaka 27 Blaise Compaoré aliyeondolewa madarakani kufuatia maandamano ya mwezi Oktoba mwa 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.