Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-COMPAORE-HAKI

Chama cha CDP chapinga mashitaka dhidi ya Blaise Compaoré

Chama cha siasa cha rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaoré cha CDP, kimeshutumu mashatika dhidi ya kiongozi huyo wa zamani.

Blaise Compaoré afunguliwa mashitaka ya kusababisha mauaji ya waandamanaji na uongozi mbaya.
Blaise Compaoré afunguliwa mashitaka ya kusababisha mauaji ya waandamanaji na uongozi mbaya. AFP PHOTO / FABRICE COFFRINI
Matangazo ya kibiashara

Compaoré ambaye aliondolewa madarakani mwaka 2014, na ambaye kwa sasa anaishi nchini Cote Dvoere anatarajwia kufunguliwa mashtaka yeye pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuiu Luc Adolphe Tiao na Waziri wake wa zamani zaidi ya 30 kwa kusababisha mauaji ya waandamanaji na uongozi mbaya.

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa tarehe 27 mwezi huu jijini Ouagadugu.

Hata hivyo, chama chake kimelaani masgtaka dhidi ya viongozi hao wa zamani na kusema ni ya kisiasa na yanakwenda kinyume na hai za binadamu.

Hata hivyo tayari baadhi ya Mawaziri wa zamani wa zamani wamefungulwia mastaka na kuachuliwa kwa dhamana lakini hawawezi kuondoka nje ya nchi hiyo.

Maandamano ya kumwondoa Compaore madaraka yalianza baada ya kuibadilisha katika na kutaka kuwania utaoia kwa muhula wa tano hata baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 27.

Watu 33 walipotez amaisha katiak maandamano hayo ya kisiasa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.