Pata taarifa kuu
ANGOLA

Watu 17 wapoteza maisha baada ya kukanyagana uwanjani nchini Angola

Watu 17 wamepoteza maisha baada ya kukanyagana katika uwanja wa michezo wa Uige Kaskazini mwa nchi ya Angola.

Gari la wagonjwa likiwasafirisha waliojeruhiwa
Gari la wagonjwa likiwasafirisha waliojeruhiwa www.thedailystar.net
Matangazo ya kibiashara

Polisi wamethibitisha kutokea kwa vifo hivyo.

Watu wengine zaidi ya mia moja wamejeruhiwa na wanaendelea kupata matibabu katika hospitali mbalimbali nchini humo.

Ajali hii ilitokea wakati mashabiki hao wa soka walipokuwa wanasukuma kuingia uwanjani kutazama mchuano wa ligi kuu kati ya Santa Rita de Cassia na Recreativo do Libolo.

Ripoti za kusikitisha zinaeleza kuwa miongoni mwa watu 17 waliopoteza maisha ni watoto ambao walishindwa kujiokoa.

Mashabiki hao walijaribu kuingia uwanjani licha ya uwanja huo kuwa umejaa na mkanyagano huo ulisababisha wengi kukosa hewa na kuzimia.

Mkasa kama huu uliwahi kushuhudiwa mwaka 2009 nchini Ivory Coast baada ya watu 19 kupoteza maisha kukanyagana jijini Abidjan wakati wa mchuano kati ya timu ya nyumbani na Malawi.

Jijini Accra nchini Ghana, hali ilikuwa kama hiyo na kusababisha watu 127 kupoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.