Pata taarifa kuu
ISRAEL-ETHIOPIA

Wayahudi 6,000 kuhamishiwa israel

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza kwamba Serikali yake imeanzisha mpango wa kuwahamishia Wayahudi wa Ethiopia nchini Israel.

Waziri Mkuu wa Israel (kushoto) na mwenzake wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn.
Waziri Mkuu wa Israel (kushoto) na mwenzake wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Takriban Waethiopia 9,000 wanaodai kuwa Wayahudi wanasubiri kuhamia Israel, na wamesubiri kwa miaka kadhaa.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu wa Israel amebaini kuwa shughuli hiyo itaanzishwa hivi karibuni.

Amesema serikali yake itahakikisha Wayahudi walioko nchini Ethiopia wanapelekwa nchini Israel kujiunga na jamaa zao ambao tayari wamefika Israel.

Inaarifiwa kuwa Wayahudi Waethiopia 130,000 wanaishi Israel kwa sasa, tangu shughuli ya kuwahamisha ianze 1984.

Waziri Mkuu wa Israel amekamilisha ziara yake barani Afrika nchini Ethiopia, baada ya kuzuru Uganda, Kenya na Rwanda

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.