Pata taarifa kuu
ISRAEL-KENYA

Netanyahu azungumzia usalama kwa kudai uwepo wa Israel Afrika

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameahidi Jumanne hii, siku ya pili ya ziara ya "kihistoria" katika ukanda wa kusini mwa Sahara, ongezeko la ushirikiano na Afrika katika kupambana dhidi ya ugaidi, akijaribu kudai uwepo wa Israel barani Afrika, ambapo kwa muda mrefu amejitenga na bara hilo.

SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kwa kufanya kazi pamoja, tunaweza kwa haraka zaidi kushinda janga la ugaidi," amesema Netanyahu katika mkutano na waandishi wa habari mjini Nairobi, baada ya mkutano na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Kutoka Kenya, mmoja wa washirika wachache wa kihistoria wa Israel barani Afrika, Netanyahu ameonyesha shauku: "Afrika haina rafiki bora nje ya Afrika kama Serikali ya Israeli wakati kunahitajika suala la mahitaji ya vitendo juu ya usalama na maendeleo. "

"Matokeo ya vitendo ya ushirikiano wetu yanaweza kuwa salama zaidi na ustawi zaidi," ameendelea Waziri Mkuu wa Israel, ambaye alishiriki Jumatatu nchini Uganda katika mkutano mdogo wa kikanda kuhusu usalama na mapambano dhidi ya ugaidi.

Kama ilivyoelezwa "kihistoria" na Bw Netanyahu, ziara ya siku nne, ambayo ilianzia Uganda na itaendelea Jumatatu nchini Rwanda na Alhamisi nchini Ethiopia ni ya kwanza kwa Waziri Mkuu wa Israel katika ukanda wa kusini mwa Sahara kwa miongo kadhaa.

Lakini kama Waziri Mkuu wa Israel amesafiri na wafanyabiashara 80, kuna haja ya mikataba na Rais wa Kenya katika urasibu wa maji, afya na uhamiaji, ziara ambayo kwa kina iliangazia mwelekeo wa kidiplomasia.

Israel inataka kuhakikisha msaada wa nchi za Afrika katika taasisi za kimataifa, ambapo Israel inakabiliwa na upinzani kuhusiana na uvamizi wa maeneo ya Palestina au kwa shughuli zake za nyuklia.

"Kama bara, tulikuwa na uhusiano mgumu na Israeli," kwa upande wake ameelezea Uhuru Kenyatta. "Lakini dunia imebadilika na hatuwezi kama siku za nyuma."

Katika miaka ya 1960, nchi nyingi za Afrika zilijitenga na Israeli kwa sababu ya vita vya Wayahudi na majirani zake kati ya mwaka 1967 na 1973 na mahusiano kati ya Tel Aviv na utawala wa kibaguzi nchini Afrika Kusini.

"Ni muhimu kwamba Israel imeanzisha uhusiano mpya na Afrika," amendelea Rais wa Kenya, wakati ambapo Israel ilikaribisha Jumatatu wiki hii katika taarifa yake, ahadi iliyochukuliwa na marais na viongozi wa serikali wa nchi za kiafrika "kuirejesha Israel kama mwanachama mwangalizi wa Umoja wa Afrika. "

Israel ilikua mwanachama mwangalizi wa Shirika la Umoja wa Afrika (OAU) mpaka mwaka 2002, wakati taasisi hii ilifutwa na nafasi yake kuchukuliwa na Umoja wa Afrika (AU).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.