Pata taarifa kuu
ISRAEL-ETHIOPIA

Benjamin Netanyahu ziarani Ethiopia

Waziri Mkuuwa Israel benjamin Netanyahu anakamilisha hatua yake ya nne na ya mwisho ya ziara yake barani Afrika. Baada ya Uganda , Kenya na Rwanda, hii leo Alhamisi Benjamin Netanyahu anaizuru Ithiopia.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akiwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda, Julai 4 2016, siku tatu kabla ya ziara yake nchini Ethiopia.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akiwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda, Julai 4 2016, siku tatu kabla ya ziara yake nchini Ethiopia. REUTERS/Presidential Press Unit/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu wa Israel anatarajiwa kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali na kutia saini mikataba kadhaa ya maendeleo.

Bw Netanyahu amesema ziara yake barani Afrika ni historia kubwa kwa Israel kufufua au kuimarisha mahusiano yake na Afrika. Israel mekua imejitenga na bara la Afrika kwa kipindi cha miaka thelathini.

Uhusiano kati ya mataifa kdhaa ya Afrika na Israel ulisitishwa mara kadhaa wakati wa vita vya Waarabu na Israel mwaka 1973. Inaarifiwa kuwa muhusiano ya kidiplomasia kati ya Etiopia na Israel yaliafikiwa upya katika miaka ya 1980 baada ya Israel na Misri kusaini mkataba wa amani mwaka 1979.

Waziri Mkuu wa Israel na mwenyeji wake wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, wanatarajiwa kuzungumzia masuala ya usalama, biashara, kilimo, elimu na mapambano dhidi ya ugaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.