Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAZUNGUMZO

Mgogoro wa Burundi: hakuna dalili ya mazungumzo Arusha

Mazungumzo kati ya serikali ya Burundi na upinzani hayatofanyika Jumatano hii, Januari 6 mjini Arusha. Tarehe hii ilipangwa na timu ya usuluhishi ya Uganda mjini Entebbe Desemba 28 mwaka uliyopita.

Ni katika mji wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania ambako kulitiliwa saini kwenye makataba uliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi viliyodumu zaidi ya mwongo mmoja.
Ni katika mji wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania ambako kulitiliwa saini kwenye makataba uliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi viliyodumu zaidi ya mwongo mmoja. © Photo: Wikimedia/Phase9
Matangazo ya kibiashara

Jumanne hii, serikali ya Bujumbura imekataa katu katu kushiriki mazungumzo hayo. Muungano wa wanasiasa waliokimbilia uhamishoni CNARED, umesema kushangazwa na uamzi huo wa serikali. Mazungumzo hayo tayari yalihirishwa mwezi Julai kwa sababu ya uchaguzi wa urais wenye utata. Hata hivyo mazungumzo hayo yalianzishwa upya mwishoni mwa mwezi Desemba nchini Uganda. Mazungumzo hayo yanaonekana kushindikana.

Hakuna tarehe mpya ya mazungumzo hayo ambayo imepangwa. Lakini kinachujulikana ni kuwa mazungumzo ya kutatua mgogoro wa Burundi hayatoanza kama ilivyopangwa Jumatano hii mjini Arusha, mahali pa ishara kwani ni katika mji huu wa kaskazini mwa Tanzania kulikotiliwa saini kwenye makubaliano yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe viliyodumu zaidi ya mwongo mmoja. "Hakutakuwa na mazungumzo kesho! Serikali ya Burundi iliiandikia barua Desemba 30 timu ya usuluhishi kutoka Uganda kwa kuiomba kuahirisha mazungumzo hadi Januari 15, tunasubiri jibu, ", amesema afisa mwandamizi katika Ofisi ya rais wa Burundi, ambaye hakutaka jina litajwe.

Tatizo la tarehe?

Waziri mkuu wa Uganda Ruhakana Rugunda, amejibu kwa umakini, akihakikisha kwamba inabidi maandalizi ya kutosha ili mazungumzo yafanyike. "Kwanza, tunapaswa kusema kwamba rais, wiki iliyopita alianzisha mazungumzo ya amani kwa Burundi katika mfumo wa majukumu aliyopewa na marais wenzake wa Afrika Mashariki. Tunafurahi kuona pande kuu husika katika mazungumzo hayo zilikuwepo, ikiwa ni pamoja na marafiki zetu wa Ulaya na Marekani. Tulikubaliana juu ya kanuni moja kwamba mazungumzo yataanzishwa rasmi mjini Arusha Januri 6, lakini yote yatategemea kwa shughuli ya maandalizi, shughuli ya kutosha. Kama shughuli ya maandalizi itakuwa bado haijakamilika vya kutosha, moja kwa moja hakutakuwa na mazungumzo mjini Arusha tarehe 6 Januari. Ni muhimu zaidi ili kuhakikisha kuwa shughuli ya kutosha kwa kuandaa mazungumzo yenye mafanikio juu ya taifa la Burundi", Waziri mkuuu wa Uganda amesema.

Mara baada ya mkutano wa Entebbe Desemba 28, serikali ya Bujumbura ilitangaza kuwa haitoshiriki katika hatua ya pili ya mazungumzo iliyopendekezwa kwa tarehe 6 Januari mjini Arusha. "Tarehe hiyo iilipangwa bila makubaliano na serikali", Ofisi ya rais wa Burundi ilirejelea kauli hii Jumanne hii.

Jérémie Minani afisa wa mawasiliano kwenye muungano wa vyama vikuu vya upinzani CNARED, ameshangazwa na uamzi huo wa serikali na kusema kuwa kuna ujanja ambao unafanyika ili kupoteza muda. "Ni njia tu ya kupotosha jumuiya ya kitaifa na kimataifa. Serikali ya Bujumbura hataki tu mazungumzo. Tatizo la makubaliano juu ya muda ni kisingizio tu", Jérémie Minani amesema.

Awali serikali ya Bujumbura ilikataa mazungumzo ya aina yoyote yatakayoishirikisha CNARED, ikishtumu wanachama wake kuhusika katika jaribio la mapinduzi la mwezi Mei.

Wapinzani upande wao, wanasema mstari mwekundu ni awamu ya tatu ya Rais Pierre Nkurunziza. "Tunakukubali mazungumzo bila masharti. Masuala yote yatajadiliwa, lakini kile ambacho CNARED haitokubali kamwe, ni makubaliano yatakayomruhusu Pierre Nkurunziza kuendelea kusalia madarakani kinyume na mihula yake miwili ambayo aliiongoza", Jérémie Minani amekumbusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.