Pata taarifa kuu
BURUNDI-JARIBIO LA MAPINDUZI

Burundi: namba 2 wa jaribio la mapinduzi "akiri kosa"

Nchini Burundi, kesi ya watuhumia wa jaribio la mapinduzi la Mei 13 mwaka 2015 imeendelea kusikilizwa Jumatatu hii katika mji wa Gitega (katikati mwa Burundi), wakati ambapo visa vya ukandamizaji kwa watu waliokua wakiandamana dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza vilikua vimekithiri.

Jenerali Cyrille Ndayirukiye (kushoto) akiwasili katika Mahakama Kuu chini Burundi iliyojielekeza katika mkoa wa Gitega, kilomita 102 na mji wa Bujumbura, Desemba 18, 2015.
Jenerali Cyrille Ndayirukiye (kushoto) akiwasili katika Mahakama Kuu chini Burundi iliyojielekeza katika mkoa wa Gitega, kilomita 102 na mji wa Bujumbura, Desemba 18, 2015. © STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa watuhumiwa waliosikilizwa ni pamoja na afisa mwandamizi mwenye cheo cha juu katika jeshi, jenerali Cyrille Ndayirukiye, ambaye "amekiri kosa".

Katika kesi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na gamu Jumatatu hii, walisikilizwa maafisa waandamizi kadhaa wa cheo cha jenerali, ikiwa ni pamoja na kiongozi namba 2 wa jaribio la mapinduzi, Cyrille Ndayirukiye, ambaye ilikuwa mara ya kwanza anasikilizwa kwa undani kuhusu tuhuma zinazomkabili. Lakini licha ya Mahakama kuchukua uamzi wa kuwafukuza wanasheria wake siku chache zilizopita, jenerali Cyrille Ndayirukiye aliwakataa wanasheria walioteuliwa na Mahakama ili waweze kumsaidia katika utetezi, na alipendelea kujitetea peke yake.

Mwanajeshi jasiri, ambaye hajakata tamaa mpaka sasa, jenerali Cyrille Ndayirukiye aliamua kukabiliana na Mahakama.

"Ninakiri kosa", jenerali Cyrille Ndayirukiye amesema mbele ya majaji.

"Singeliweza kukaa kimya wakati ambapo polisi ilikua ikiua raia bila hofu yoyote, huku rais Pierre Nkurunziza akicheza mpira, na askari, wakisubiri kupelekwa kusimamia amani nchini Somalia, wakiwa katika hali ya mtafaruku mkubwa.", jenerali Ndayirukiye ameeleza mbele ya majaji.

Waziri wa zamani wa ulinzi wa Burundi amekubali kuhusika katika jaribio la mapinduzi la tarehe 13 na 14 Mei katika kilele cha maandamano dhidi ya awamu ya tatu ya Nkurunziza.

"Lengo letu lilikuwa kuheshimisha Mkataba wa Amani wa Arusha na katiba ya Burundi ambavyo vilikiukwa", jenerali Ndayirukiye amesisitiza.

Jenerali Cyrille Ndayirukiye pia amesema kuwa yeye na wenzake wafungwa alikataa kubeba mzigo peke yake. Na Hivyo ameomba, kama anavyofanya tangu kukamatwa kwake, waziri wa ulinzi wakati huo jenerali Pontien Gaciyubwenge ambaye yuko uhamishoni, au pia Mkuu wa sasa wa majeshi, jenerali Prime Niyongabo wafikishwe mahakamani ili waweze kuulizwa kuhusu jaribio hilo, akibaini kwamba maafisa hao ni "miongoni mwa waliopanga jaribio hilo la mapinduzi kabla kubadili msimamo".

Mamia kwa maelfu ya waafuasi wa upinzani wamepongeza "ujasiri" wa mwanajeshi huyo kwenye mitandao ya kijamii. Kwa upande wake mshauri mkuu wa rais Willy Nyamitwe, amesema kwenye Tweeter kuwa "haiwezekani kulindia usalama raia kwa kukiuka uhuru wao".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.