Pata taarifa kuu
CAR-UCHAGUZI-SIASA

CAR: Chama cha Bozizé chatoa wito wa kumpigia kura Dologuélé

Chama cha siasa cha Rais wa zamani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati François Bozizé, cha Kwa Na Kwa, kimetangaza Jumanne hii kuunga mono kugombea kwa Waziri mkuu wa zamani Anicet-Georges Dologuélé Jumapili mwishoni mwa wiki hii.

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, François Bozizé.
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, François Bozizé. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Anicet-Georges Dologuélé, ambaye aliteuliwa na chama chake cha URCA kugombea katika uchaguzi wa rais, alihudumu kama waziri mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwaka 1991 hadi mwaka 2001.

Kwa upande mwingine, kiongozi wa waasi Noureddine Adam, ambaye alitangaza mwezi huu ujio wa taifa huru katika maeneo yalio chini ya utawala wake, amerejelea msimamo wake wa kupinga uchaguzi huo mkuu wa urais na ubunge, utakaofanyika Jumapili mwishoni mwa wiki hii.

"Kundi letu limeamua kuchangia vyema na kwa moyo wa dhati katika zoezi la uchaguzi kwa utulivu, amani, bila vurugu na kwa ushiriki mkubwa", imesomwa katika taarifa, iliyotolewa na Ofisi ya rais wa Chad, ambaye alikua na jukumu la upatanishi pamoja na Adam.

François Bozizé alitimuliwa madarakani mwanzoni mwa mwaka 2013 wakati waasi wa Kiislamu wa kundi la Seleka walipochukua madaraka nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, nchi yenye Wakristo wengi. Vurugu za waasi hao walizofanya zilisababisha kundi la wanamgambo la Kikristo la Anti-Balaka kujilipiza kisasi, na hivyo kuitumbukiza koloni hiyo ya zamani ya Ufaransa katika ghasia za kikabila.

François Bozizé ambaye anaishi uhamishoni nchini Uganda kwa muda mrefu tangu kuangushwa kwake madarakani, alijikuta uamuzi wake wa kugombea katika uchaguzi wa urais wa Desemba 27, ukikataliwa na Mahakama ya Katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.