Pata taarifa kuu
CAR-UCHAGUZI-SIASA

CAR mbioni kuanza mchakato wa uchaguzi

Uchaguzi mkuu nchini Jamahuri ya Afrika ya Kati utafanyika tarehe 13 mwezi Desemba mwaka huu, baada ya nchi hiyo miezi kadhaa nchi hiyo kukumbwa na machafuko yaliyosababisha vifo vya watu wengi na wengine kulazimika kuyahama makaazi yao..

Catherine Samba Panza.
Catherine Samba Panza. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Tarehe hiyo imetangazwa na tume ya Uchaguzi na kurejesha matumaini ya kurejeshwa kwa hali ya kidemokraia nchini humo tangu mwaka 2013.

Uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu lakini ukaahirishwa kwa sababu ya machafuko yaliyozuka jijini Bangui.

Mzunguko wa pili wa uchaguzi wa urais utafanyika tarehe 24 mwezi Januari ikiwa mshindi hatapatikana katika mzunguko wa kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.