Pata taarifa kuu
RCA-MACHAFUKO-USALAMA

RCA: machafuko mapya yatokea Bangui

Watu wanne wameuawa Jumapili hii iliyopita katika machafuko mapya kati ya makabila yaliyotokea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, siku moja baada ya makabiliano yaliyosababisha watu 21 kuuawa na wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa, vyanzo vya hospitali vimebaini.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakipiga doria katika mji wa Bangui, wakisaidiwa na vikosi vya Ufaransa (Sangaris).
Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakipiga doria katika mji wa Bangui, wakisaidiwa na vikosi vya Ufaransa (Sangaris). .FP PHOTO / REINNIER KAZE
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya mpito imethibitisha kwamba watu walioandaa vurugu hizo walikua na lengo la kuzuia uchaguzi uliyopangwa kufanyika mwezi ujao. Serikali imechukua hatua ya kutotoka nje usiku kuanzia saa 12 jioni hadi saa 12 asubuhi.

Wanamgambo wa kikristo ambao wamekua wakibebelea silaha za kivita na mapanga waliingia mitaani Jumapili hii katika mji mkuu Bangui ambapo waliweka vizuizi barabarani.

Katika masaa ya mwanzo ya Jumapili hii, vijana wenye hasira walizuia barabara ya kuingia mjini Bangui kwa mashina ya miti. Wanajeshi wa vikosi vya Umoja wa Mataifa, Minusca, walijaribu kuwatawanya vijana hao wa kikristo katika mtaa wa Bogenda kwa kurusha gesi za kutoa machozi, bila mafanikio.

Mashahidi wamebaini kwamba wamesikia milio mingi ya risasi katika baadhi ya maeneo na kushuhudia visa vya uporaji katika nyumba mbalimbali na maduka.

Machafuko ya Jumamosi yaliendeshwa na Waislam walioghadhabishwa na mauaji ya ndugu yao aliyeuawa katika mji wa Bangui.

Haya ni machafuko mabaya kabisa kushuhudiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu katika mji wa Bangui, ambapo vikosi vya Ufaransa, na walinda amani wa Umoja wa Mataifa wameendelea kuimarisha usalama.

Waislam waliondoka katika eneo wanakoishi katika mtaa wa tatu mjini Bangui na kwenda kushambulia kwa risasi wakazi wa mtaa wa tano wanakoishi Wakristo wengi, ambapo nyumba na magari vilichomwa moto. Maelfu ya wakazi walilazimika kukimbilia katika maeneo jirani ya mji huo.

Makao makuu ya kituo cha redio cha Waislam, Sauti ya Amani, na Kanisa ya mtaa wa tano mjini Bangui ni miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.