Pata taarifa kuu
BANGUI

Machafuko mapya yaripotiwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mtu mmoja ameuawa na wangine 10 kujeruhiwa katika makabiliano ya kidini ya hivi punde nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

AFP Photo/Edouard Dropsy
Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka jijini Bangui zinasema makabiliano yalianza kushuhudiwa siku ya Alhamisi katika ngome ya Waislamu na kusababisha maelfu ya watu kuyakimbia makwao.

Inaripotiwa kuwa baadhi ya watu wamerejea makwao siku ya Ijumaa baada ya kuripotiwa kuwepo kwa hali ya utulivu kuanza kurejea.

"Makabiliano haya yalizuka baada ya kuuawa kwa kijana wa Kiislamu anayetuhumiwa kuuawa na waasi wa Anti-Balaka ambao ni Wakiritso,” mwenyeji mmoja amesema.

Anti Balaka “ Baadaye walianza mashambulizi na kuanza kukabiliana na vijana wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa silaha.”

Inahofiwa kuwa idadi na vifo huenda ikaongezeka na baadhi ya watu wamekuwa wakinukuliwa wakisema watu waliopoteza maisha ni watatu.

Makabiliano haya ya hivi punde yanakuja baada ya watu 61 kuuawa mwezi uliopita na zaidi 300 kujeruhiwa baada ya makabiliano mengine kuzuka kabla ya kutulizwa na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Machafuko ya hivi karibuni yamesababisha uchaguzi wa urais na ule wa wabunge uliokuwa umeratibiwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu wa Oktoba kuahirishwa.

Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu 460,000 wameikibia nchi hiyo na wanapewa hifadhi nchini Cameroon, Chad na DRC tangu mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.