Pata taarifa kuu
BURUNDI-EAC-USALAMA-SIASA

Burundi: Warundi watarajiye nini kutoka kwa mpatanishi mpya Yoweri Museveni?

Rais Museveni aliyeteuliwa Julai 6 kama mpatanishi mpya katika mkutano wa kilele wa mwisho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Dar es Salaam, amewasili leo Jumanne nchini Burundi.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameteuliwa kuwa mpatanishi kwa Burundi Julai 6. Hapa kwenye picha, ni katika mkutano wa Umoja wa Afrika mwaka 2014.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameteuliwa kuwa mpatanishi kwa Burundi Julai 6. Hapa kwenye picha, ni katika mkutano wa Umoja wa Afrika mwaka 2014. Reuters/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya kikazi ya masaa 24, ikiwa zimesalia siku sita kabla ya uchaguzi wa urais unao leta utata. Upinzani ulilani na kutupilia mbali maazimio ya mkutano huo, ukitaja kwamba unamtetea rais Nkurunziza. Kambi ya rais ulikaribisha maazimio hayo. Nini cha kutarajia kutoka kwa rais wa Uganda?

Kitu gani kweli Yoweri Museveni anaweza kukamilisha ndani ya masaa 24? Vigumu kusema. Jumuiya ya Afrika Mashariki imepanga mfululizo wa matukio: mkutano na marais wa zamani, vyama vya siasa na viongozi wa dini. Lakini anaweza kuibadili ratiba hiyo kulingana na matakwa yake, ameeleza afisa mmoja wa Afrika Mashariki.

Hatimaye, wanasiasa wote kutokana vyama mbalimbli wameonekana kupigwa na mshangao. Upande wa chama tawala na upinzani, wamesema wanasubiri na kuona nini ujumbe wake. Uchaguzi wa urais umepangwa rasmi kufanyika tarehe 21 Julai , yaani wiki moja tu ndio inayosalia. Mkutano wa kilele wa mwisho wa Dar es Salaam ulipendekeza kuahirushwa kwa uchaguzi hadi Julai 30. "Ilikuwa mapendekezo na wala si amri. Ilikuwa inatakiwa rais wa Burundi aheshimu Katiba ", amesema Willy Nyamitwe, Mshauri mkuu wa rais katika masuala ya Mawasiliano.

Ni hatari, upinzani umejibu. Upinzani unakusudia kuomumba rais wa Uganda kurudi kwenye mapendekezo na muuongozo wa Umoja wa Afrika: mazungumzo bila miiko, ikiwa ni pamoja na awamu ya tatu, ufafanuzi wa makubaliano wa tarehe ya uchaguzi mpya. Upinzani unajiandaa kukutana na rais Yoweri Museveni. Leonce Ngendakumana, kiongozi wa mmungani wa vyama vikuu vya upinzani ADC-Ikibiri, inaeleza kwa nini: " Tutakutana naye kwa mazungumzo, tutamsikiliza, tusikie ujumbe wake kwa sababu hatujui mpaka sasa ajenda mkutano. Tutamsikisikiliza na tutamuonyesha hali halisi ya mambo inayojiri hapa nchini. Na tutatoa msimamo wetu. Tunatarajia mengi kwa Museveni, si kama msuluhishi lakini kama msimamizi wa Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha, kwani yeye ndiye alikuwa rais wa jitihada za kikanda kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba huu. Hivyo sisi tunatarajia msaada wake kwa kutetea Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha. "

Kambi ya rais inataka kuona kwa upande wake, Museveni anafaulu kuushawishi upinzani ili ushiriki katika uchaguzi ujao na ukubali matokeo ya uchaguzi uliopita.

Rais yoweri Kaguta Museveni amewasili mjini Bujumbura mchana tofauti na asubuhi kamailivyokua kwenye ratiba.

Uamzi wa kubadili ratiba hiyo imechukuliwa na itifaki yake katika dakika za mwisho. Rais Yoweri Kaguta Museveni ameingia nchini Burundi kwa gari akipitia mkoani Kirundi Kaskazini mwa Burundi, kwenye mpaka na nchi ya Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.