Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA-SIASA

Burundi: Silaha kadhaa zakamatwa, upinzani wanyooshewa kidole

Baada ya kundi la watu wenye silaha kuingia nchini na kukabiliana na jeshi siku tatu zilizopita katika mkoa wa Kayanza, Kaskazini mwa Burundi, Jumapili Julai 12 polisi imefaulu kukamata bunduki thelathini katika kijiji kimoja cha mkoa wa Muyinga, Kaskazini Mashariki mwa nchi.

Watu wote waliokamatwa ni wafuasi wa chama cha upinzani cha FNLkinachoongozwa na Agathon Rwasa (picha), mmoja wa wapinzani wakuu Burundi.
Watu wote waliokamatwa ni wafuasi wa chama cha upinzani cha FNLkinachoongozwa na Agathon Rwasa (picha), mmoja wa wapinzani wakuu Burundi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wafuasi thelathini wa upinzani wamekamatwa kufuatia kukamatwa kwa silaha hizo. Utawala umethibitisha kukamatwa kwa silaha hizo. Kugunduliwa kwa silaha hizo kulitokea tu ghafla, polisi mkoani Muyinga imebaini.

Inaarifiwa kuwa Jumapili asubuhi mwishoni mwa juma hili vijana kutoka chama tawala nchini Burundi cha Cndd-Fdd, Imbonerakure mkoani Muyinga, walimsimamisha ghafla mwendesha pikipiki ya kukodiwa ambaye alikua alibeba mfuko wa mbegu za viazi utamu. Walipofungua mfuko huo ndipo kugundua silaha kumi na visanduku 38 vya risasi, kwa mujibu wa vyanzo vya polisi.

Vijana hawa kutoka chama tawala walikabidhi silaha hizo polisi, ambayo papo hapo iliamua kuendesha msako katika kijiji hicho cha mkoa wa Muyinga, kilomita 280 Kaskazini Mashariki mwa mji mkuu wa Burundi, Bujumbura. Katika msako huo, bunduki ishirini zilikamatwa, ameeleza mkuu wa mkoa wa Muyinga, Aline Manirabarusha.

" Hii haijawahi kutokea. Msako kabambe ambao haujawahi kufanywa na polisi na kufaanikiwa kukamata silaha kama hizi katika historia ya Burundi ", amesema mkuu wa mkoa wa Muyinga.

Baada ya msako huo polisi iliwaweka nguvuni watu 31, ambao wote ni kutoka chama cha upinzani cha FNL kinachoongozwa na Agathon Rwasa.

" Watu hawa walikuwa katika orodha ya kundi la watu waliokua wamedhamiria kuhatarisha usalama, orodha ambayo ilipatikana katika eneo kulikoendeshwa msako ", amethibitisha mkuu wa mkoa wa Muyinga. Lakini katika kambi ya Agathon Rwasa, wanakanusha tuhuma hizo. Wamesema ni mpango ulioandaliwa na utawala ili kukivunja chama kikuu cha upinzani.

Hayo yakijiri mapigano yanaendelea kati ya kundi la watu wenye silaha na vikosi vya usalama na jeshi katika mikoa ya kaskazini mwa Burundi, hususan katika msitu wa Kibira. Hata hivyo jeshi limebaini kwamba limedhibiti hali ya mambo na limefanikiwa kulivunja kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.