Pata taarifa kuu
AFRIKA-LIBYA-ITALIA-WAHAMIAJI-AJALI

Italia yatoa wito wa kufanyika mkutano wa dharura

Zaidi ya wahamiaji 11,000 waliokuolewa kwa kipindi cha wiki moja, huku zaidi ya wahamiaji 700 wakifariki kufuatia kuzama kwa meli waliyokuwemo usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita katika pwani ya Libya.

Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi katika mkutano na vyombo vya habari, Aprii 19 mwaka 2015.
Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi katika mkutano na vyombo vya habari, Aprii 19 mwaka 2015. REUTERS/Tony Gentile
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya wanakutana leo Jumatatu Aprili 20 mjini Luxemburg ili kujadili hali hiyo.

Italia inahisi kuwa peke yake kwa kukabiliana na tatizo hili la kuongezeka kwa vifo vya wahamiaji kutokana na kuongezeka kwa matukio ya kuzama kwa meli zinazowasafirisha katika bahari ya Mediterranean. Serikali ya Italia imeoa wito wa kufanyika kwa mkutano wa dharura wa Umoja wa Ulaya.

Kufuatia hali hiyo, Roma imetoa wito wa haraka ili Italia isiendelei kubeba mzigo peke yake, mzigo ambao usiyobebeka. Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi ameomba kufanyika kwa mkutano wa dharura wa Umoja wa Ulaya, akibaini mbele ya vyombo vya habari kwamba huenda matukio hayo yakaongezeka siku za usoni.

Kuhusu tukio mpya la kuzama kwa meli katika pwani ya Libya, ambayo inadaiwa kuwa wahamiaji 700 walifariki usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita, waziri mkuu wa Italia, amebaini kwamba kilichotokea katika bahari ya Mediterranean sio janga bali ni mauaji.

“ Kila siku katika bahari ya Mediterranean, tunashuhudia mauaji ya wanaume na wanawake wengi, ambao tumekua tukiwasahau”, amesema Matteo Renzi.

“ Ndugu zetu na dada zetu wamekua wakiokolewa na kikosi cha majini peke yake, kwa hiyo haitakiwi tuwaache waangamizwe na wafanyabiashara haramu wa watu”, ameongeza waziri mkuu wa Italia.

Baada ya taarifa hiyo ya huzuni ya kufariki kwa wahamiaji 700 katika pwani ya Libya, hisia mbalimbali zilitolewa na viongozi wa Ulaya wakidai kwamba kuna ulazima kuboresha ushirikiano na nchi ambazo wahamiaji hao hutokea pamoja na nchi wanakopitia hususan Libya.

Waziri mkuu wa Italia amesema moja ya malengo ya mkutano huo ni kupambana dhidi ya biashara haramu ya watu, huku ulinzi mkali ukitolea katika bahari ya Mediterranean.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.