Pata taarifa kuu
UFRANSA-ALGERIA-Mateka-Mauaji

Ufaransa: maandamano ya waislam dhidi ya mauaji ya Hervé Gourdel

kuandamana ijuma wiki hii nje ya Msikiti mkuu kulaani kuuliwa kwa kukatwa shingo raia wa nchi hiyo, Hervé Gourdel.

Bakr al-Baghdadi. Ảnh ghi ngày.
Bakr al-Baghdadi. Ảnh ghi ngày. REUTERS/Social Media Website via Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Mauaji ya raia huyo wa Ufaransa yaliyotekelezwa juma hili na wapiganaji wa Kiislamu nchini Algeria wanaoshirikiana na wapiganaji wa Islamic State.

Rais Francois Hollande ameagiza bendera kupeperushwa nusu mlingoti kuanzia leo Ijumaa kwa kipindi cha siku tatu kuomboleza kifo cha Goudel.

Kutokana na tukio hilo, serikali imetanagza kuimarisha usalama katika maeno yote ya umma.

Kundi la Jund al-Khalifa linaloongozwa na Abou Souleimane Khaled akijulikana kwa jina lake halisi la Abdelmalek Gouri linadaiwa kuhusika na mauwaji ya Hervé Gourdel. Kundi hilo linaendesha harakati zake nchini Algeria katika jimbo la Kabylie, limekua likitekeza mashambulizi mbalimbali nchini humo.

Mwezi Julai Jund al-Khalifa lilitangaza kuungana na wapiganaji wa Dola la Kiislam, na kukubali kuwa wawakilishi wa Doal hilo ncvhini Algeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.