Pata taarifa kuu
NIGERIA

Mshukiwa wa Boko Haram akamatwa baada ya shambulizi la Bomu jijini Abuja

Polisi nchini Nigeria wamemkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kutekeleza shambulizi katika duka la jumla jijini Abuja siku ya Jumatano na kusababisha vifo vya watu 21 na wengine kujeruhiwa.

Shambulizi katika jengo la biashara la  Emab Plaza jijini Abuja.
Shambulizi katika jengo la biashara la Emab Plaza jijini Abuja. AP
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Boko Haram lilitokea katika duka la Emab Plaza saa 10 jioni wakati wakaazi wa jiji hilo walipokuwa wanafanya manunuzi ya bidhaa kabla ya kwenda nyumbani.

Msemaji wa polisi nchini humo Frank Mba amethibitisha kukamatwa kwa mshukiwa mmoja, na kuongeza kuwa watu waliojeruhiwa ni 17.

Hasara baada ya shambulizi la Abuja
Hasara baada ya shambulizi la Abuja REUTERS/Stringer

Kituo cha kitaifa kinachoshughulikia maswala ya Habari kinasema mshukiwa mwingine alipigwa risasi hadi kufa na polisi wakati alipokuwa anatoroka.

Kundi la kigaidi la Boko Haram limekuwa likitishia kuendeleza mashambulizi zaidi nchini humo wakati huu, jeshi likiendelea na Operesheni ya kuwasaka wasichana zaidi ya 200 waliotekwa na kundi hilo.

Mwezi Aprili mwaka huu, kundi la Boko Haram lilivamia kituo cha basi cha Nyanya na kutekeleza watu 75 na baadaye kukatokea na shambulizi lingine papo hapo na kusababisha watu 19 kupoteza maisha.

Mwanamke akiokolewa jijini Abuja
Mwanamke akiokolewa jijini Abuja REUTERS/Afolabi Sotunde

Idadi kubwa ya raia nchini Nigeria wameilaumu serikali ya rais Goodluck Jonathan kwa kushindwa kukabiliana na kundi hilo la Boko Haram ambalo limeendelea kutekeleza mashambulizi nchini humo.

Juma hili, Boko Haram liliripotiwa kuwateka zaidi ya wanawake na wasichana 80 katika jimbo la Borno na kuwapeleka kusikojulikana.

Boko Haram inasema iko tayari kuwaachilia wasichana hao ikiwa serikali ya Nigeria itawaachilia wanachama wake, suala ambalo serikali ya Nigeria imekataa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.