Pata taarifa kuu
NIGERIA

Boko Haram wawateka nyara tena wanawake na wasichana wengine 60 Nigeria

Kundi la kigaidi la Boko Haram nchini Nigeria, kwa mara nyingine limewateka nyara zaidi ya wanawake na wasichana 60 katika jimbo la Borno Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wanamgambo wa Boko Haram
Wanamgambo wa Boko Haram AFP PHOTO/YOUTUBE
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wasichana waliotekwa nyara wana umri wa miaka mitatu na utekaji nyara huu unafanyika mwezi mmoja na nusu baada ya kundi hilo pia kuwateka wasichana wa shule zaidi ya 200 katika mji wa Chibok katika jimbo hilo.

Utekaji nyara huu mpya umefanyika katika kijiji cha Kummabza katika Wilaya ya Damboa unaelezwa na wachambuzi wa maswala ya usalama kama mbinu ya Boko Haram kuendeleza shinikizo zao kwa serikali ya Nigeria kutaka kuachiliwa huru wapiganaji wao.

Baadhi ya wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram
Baadhi ya wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram

Kundi la Boko Haram tayari limeweka wazi kuwa liko tayari kuwaachilia huru wasichana wa shule waliowateka nyara ikiwa wapiganaji wake wataachiliwa huru, shinikizo ambazo rais Goodluck Jonathan amesema serikali yake haiwezi kutekeleza.

Jeshi nchini Nigeria ambalo linasema linaendelelea na Operesheni maalum ya kuwaokoa wasichana waliotekwa nyara mwezi Aprili linasema haliwezi kuthibitisha utekwaji nyara huu mpya.

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau As received by Reuters

Aji Khalil, kiongozi wa kundi la vijana wanaopambana na Boko Haram amelimbia Shirika la Habari la AFP kuwa “ Zaidi ya wanawake 60 walitekwa na wanamgambo wa Boko Haram na walilazimishwa kuandama nao,”.

“Wanawake wanne walijaribu kutoroka lakini wakapigwa risasi na kuuawa papo hapo na wanamgambo hao,” aliongezea.

Mkaazi mwingine wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema wanaume zaidi ya 30 waliuliwa wakati wa utekaji nyara huo.

Wanaharakati nchini Nigeria wakishinikiza kuachiliwa huru kwa wasichana wa shule
Wanaharakati nchini Nigeria wakishinikiza kuachiliwa huru kwa wasichana wa shule REUTERS/Afolabi Sotunde

Nigeria imekuwa ikishtumiwa na raia wake kwa kushindwa kuwaokoa wasichana hao licha ya kupata msaada kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.