Pata taarifa kuu
NIGERIA

Boko Haram washambulia tena jimbo la Yobe nchini Nigeria

Watu wasiopungua 21 wameuawa usiku wa kuamkia leo jumatano katika Shambulio lililotokea katika jimbo la Yobe huko kaskazni mwa nchi ya Nigeria wakati wakitazama mechi kati ya Brazil na Mexico, vyanzo vya madaktari vimeripoti  nchini humo.

Kiongozi wa kundi la Boko haram, Abubakar Shekau March 24, 2014
Kiongozi wa kundi la Boko haram, Abubakar Shekau March 24, 2014 (Boko Haram/AFP)
Matangazo ya kibiashara

Kufwatia mashambulizi yanayotekelezwa na kundi wapiganaji Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo maafisa wa usalama waliamua kuliweka Jimbo hilo katika hali ya hatari hasa katika kipindi hiki cha kombe la dunia, kujaribu kukabiliana na mashambulio ya kundi hilo.

Madaktari wanasema walipokea miili ya watu 21, pamoja na majeruhi 27 mara baada ya kutokea mlipuko mkubwa nje ya eneo la kutazama sinema mjini Damaturu katika kata ya Nayi Nama, ambapo mashabiki wa soka walikua wamejumuika kutazama mechi za kombe la dunia.

Mashahidi wanasema walimuona mshambuliaji mmoja wa kujitolea muhanga na ambaye alikuwa amebebwa kwa baisikeli akikaribia mgahawa walikokuwa wamejazana watu kutazama mechi.

Duru kutoka hospitalini zinasema kuwa waliopelekwa hapo wana majeraha mabaya huku baadhi yao wakipoteza miguu na mikono.

Serikali ya nigeria imethibitisha kuwa mashambulio hayo yametekelezwa na kundi hilo la Boko Haram kufwatia kuwa siku kadhaa zilizopita kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau alielezea mpira wa miguu ni jambo ambalo linapotosha watu wengi na linalenga kurudisha nyuma dini ya Kiislamu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.