Pata taarifa kuu
Nigeria

Watu 15 wauawa katika shambulio lililotekezwa na Boko Haram nchini Nigeria

Watu takribani kumi na watano wameuawa nchini Nigeria katika shambulizi linalodaiwa kuwa lilitekelezwa na wapiganaji wa kundi la Boko Haram dhidi ya soko iliyoko kaskazini mwa nchi hiyo.Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa waliona kundi la watu waliojihami kwa silaha na mapanga ambao walikuwa wamejifunika nyuso zao wakiingia katika soko hilo jana jumapili majira ya jioni.

Wapiganaji wa Kundi la Boko Haram nchini Nigeria
Wapiganaji wa Kundi la Boko Haram nchini Nigeria AFP PHOTO/YOUTUBE
Matangazo ya kibiashara

Wakaazi wa mji wa Daku katika jimbo la Borno walionusurika katika shambulio hilo, wamewaambia wanahabari waliozuru eneo la tukio hii leo jumatatu kuwa walizingirwa na watu wasiopungua ishirini, ambao walianza kuwafyeturia risasi za moto.

Mfanyabiashara aliyejitambulisha kama Laraba Simon anasema, siku ya jumapili ni siku inatambulikana na watu wengi kuwa ndio siku ya soko maalum ya mji huo, ambapo mara nyingi watu kutoka vijiji jirani wanakuja kununua bidhaa muhimu na chakula ndani ya soko hilo.

Zaka samaila ni mkaazi wa maeneo jirani na soko hilo, anasema mara baada ya wapiganaji hao Boko Haram kuingia walianza kurusha mabomu na kufyetua risasi kiholela na baadaye kuteketeza kwa moto sehemu kubwa ya soko hilo.

Wakaazi wanasema miili ya watu ikiwemo na moja ya kiongozi wa mji huo, ilionekana ndani ya msitu unaozingira soko hili, na kwamba kutokana na ukubwa wa hasara kuna uewzekano wa kuongezeka kwa idadi ya watu waliopoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.