Pata taarifa kuu
KENYA

Watu 11 wauliuwa katika mashambulizi mapya Pwani ya Kenya

Polisi Pwani ya Kenya wanasema watu waliojihami kwa silaha wamevamia kijiji cha Witu na kuwaua watu 11 , juma moja tu baada ya watu wengine wasiojulikana kuvamia eneo la Mpeketoni na kuwaua watu zaidi ya sitini.

Wakaazi wa Mpeketoni wakiandamana baada ya mauaji ya juma lililopita
Wakaazi wa Mpeketoni wakiandamana baada ya mauaji ya juma lililopita REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kamishena wa Kaunti ya Lamu Stephen Ikua amethibitisha kutokea kwa mashambulizi hayo usiku wa kuamkia siku ya Jumanne na kusema yalikuwa yakusikitisha.

Naibu Kamishena katika kauti hiyo Benson Maisori amesema baadhi ya watu waliopoteza maisha baada ya kudungwa visu, huku wengine wakipigwa risasi na wengine kujeruhiwa.

Mauaji haya yanakuja juma moja baada ya kutokea kwa mauaji mengine ya watu sitini katika vijiji vya Mpeketoni, mauaji ambayo serikali ilisema yalipangwa na kuchochewa kisiasa.

Hata hivyo, kundi la kigaidi la Al Shabab lilikiri kutekeleza mashambulizi hayo kutokana na serikali ya Kenya kuendelea kuwa na wanajeshi wake nchini Somalia.

Hasara baada ya mashambulizi ya Mpeketoni
Hasara baada ya mashambulizi ya Mpeketoni

Upinzani nchini Kenya umekuwa ukiishinikiza wakuu wa usalama nchini humo kujiuzulu kwa kushindwa kuwalinda wakenya na kuwahakikishia usalama wao katika siku za hivi karibuni.

Inspekta wa Polisi David Kimaiyo alinukuliwa juma hili akisema hawezi kujiuzulu kwa kile alichokisema kuwa mauaji hayo yangezuiliwa kama sio kupangwa na kochechewa kisiasa.

Maeneo mengi ya Pwani nchini Kenya yamekuwa yakishuhudia mzozo wa ardhi kutokana na wenyeji wa eneo hilo kudai kuwa ardhi yao imenyakuliwa na wageni.

Mauaji ya juma lililopita yalilenga jamii moja ambayo ilihamia katika eneo la Mpeketoni miaka ya sabini wakati wa uongozi wa rais wa kwanza wa taifa hilo Jomo Kenyatta ambaye alikuwa baba wa rais wa sasa Uhuru Kenyatta.

Mauji ya Mpeketoni
Mauji ya Mpeketoni Reuters

Kuzorota kwa usalama Pwani ya Kenya tangu mashambulizi ya kigaidi ya Al Shabab yalipoanza nchini humo umesababisha nchi ya Uingereza kufunga Ubalozi wake mdogo mjini Mombasa na kuwawaomba raia wake kutozuru Pwnai ya Kenya.

Mataifa mengine ambayo pia yamewarai raia wake kuwa makini wanapozuru Pwani ya Kenya ni pamoja na Ufaransa na Marekani.

Siku ya Jumatatu Jeshi la Umoja wa Afrika AMISOM linalopambana na wanagambo wa Al Shabab nchini Somalia lilisema kuwa, jeshi hilo likiongozwa na lile la Kenya KDF lilitekeleza mashambulizi katika ngome za kundi hilo Kusini mwa Somalia na kuwaua zaidi ya wanamgambo 80.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.