Pata taarifa kuu
KENYA

Upinzani nchini Kenya umekanusha kuhusika kwa namna yeyote na mashambulizi ya Mpeketoni

Upinzani ukiongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga umekanusha kuhusika kwa namna yeyote na mashambulizi yake na badala yake inasema serikali ya rais Kenyatta aimeshindwa kuwalinda wakenya na badala yake inawalaumu bure.Hata hivyo, serikali ya Kenya inakunusha madai ya Al Shabab kuwa ilitekeleza mashambulizi hayo na badala yake inasema yalichochewa kisiasa.

STANDARD News
Matangazo ya kibiashara

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa, mauaji hayo yalipangwa na kuchochewa kisiasa kwa kuwa ujasusi ulipata taarifa za awali kuhusu kufanyika mashambulizi hayo, bali havikuchukua tahadhari.

Maafisa wakuu wa mashirika ya ujasusi waliohusika wameachishwa kazi huku serikali ikielezea kuwa watashitakiwa mbele ya mahakama.

Hata hivyo Raisi Kenyatta amesema kuwa maafisa wakuu wa kijeshi na wengine kutoka vyombo vya dola wanachunguza wanasiasa waliohusika na mauaji hayo.

Wadadisi wa maswala ya Usalama wanasema kuwa kauli ya rais Kenyatta ni ya kupotosha na kusisitiza kuwa mfumo wa kiusalama nchini humo ndio wenye kukabiliwa na matatizo.

Chama cha Mawakili nchini Kenya LSK kimeungana na upinzani pamoja na Mashirika ya kiraia kuendelea kumshinikiza Waziri wa Usalama nchini humo Josep Ole Lenku kujizuulu, kutokana na mashambulizi ya Mpeketoni Pwani ya Kenya ayaliyosabisha zaidi ya watu 60 kupoteza maisha.

Ole Lenku sasa amepewa wiki mbili kuacha kazi, la sivyo atafikishwa Mahakamani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.