Pata taarifa kuu
HAKI ZA BINADAMU

Wanaharakati wachukizwa na hatua ya China na Urusi kupata nafasi kwenye tume ya haki za binadamu

Kumeripotiwa maandamano makubwa kwenye mataifa mbalimbali wanachama wa Umoja wa Mataifa UN kupinga hatua ya baadhi ya mataifa yanayodaiwa kukithiri kwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu kujumuishwa kwenye baraza la tume ya haki za binadamu ya umoja huo.

Baadhi ya waandamanaji wakiwa nje ya ukumbi wa Umoja wa Matiafa kupinga nchi za China na Urusi kujumuishwa kwenye tume ya haki za binadamu
Baadhi ya waandamanaji wakiwa nje ya ukumbi wa Umoja wa Matiafa kupinga nchi za China na Urusi kujumuishwa kwenye tume ya haki za binadamu UN
Matangazo ya kibiashara

Nchi za Uchina, Urusi, Saudi Arabia na Cuba zimeshinda nafasi ya kuwemo kwenye baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, uteuzi ambao umekosolewa kwa sehemu kubwa na wanaharakati wa haki za binadamu duniani.

Nchi kumi na nne ziliteuliwa kuunda baraza la tume ya haki za binadamu kwenye umoja wa mataifa, tume ambayo itakuwa na wajumbe arobaini na saba huku ikikabiliwa na jukumu la kuhakikisha amani inarejea nchini Syria.

Baraza hilo la tume ya haki za binadamu linatarajiwa kuanza kazi yake mwezi January mwakani, huku wajumbe wake wakielezwa kuwa ni sehemu ya mataifa yaliyokithiri kwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.

Wanaharakati wanahoji uhalali wa China kujumuishwa kwenye baraza hilo wakati inatuhumiwa kuwanyanyasa wananchi wake pamoja na wanaharakati ambao wamekuwa wakosoaji wa kubwa wa utawala.

Nchi ya Urusi nayo haikuachwa kwenye ukosolewaji huu ikituhumiwa kugandamiza uhuru wa wanasiasa nchini humo na hasa wanaokosoa utawala.

Nchi ya Saudi Arabia nayo imekosolewa kwa sehemu kubwa kuwemo kwenye tume hiyo kwa kile wanaharakati wanadai kuwa inawanyima haki wanawake hasa kwenye sheria yake ya kuwakataza wanawake kuendesha magari.

Nchi za Ufaransa na Uingereza zenyewe zimerejea tena kwenye tume hiyo huku nchi za Afrika Kusini, Vietnam, Algeria, Morocco, Namibia, Maldives, Macedonia na Mexico zikifanikiwa kushika nafasi hiyo kwa muhula wa miaka mitatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.